Morali Imekata Kabisa

kasanga70

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
227
Reaction score
517
Wasalaam

Takribani miaka 25 iliyopita nilikuwa natamani sana kufahamu mama Tanzania amebeba matarajio yangu ya kimaisha kwa kiasi Gani.

Nilifatilia sana siasa za nchi yangu, nilijihusisha na siasa, nilifatilia bunge jeshi letu,watu maarufu viongozi wa siasa n.k nilitamani wawe role model wangu nk.

Mambo yamebadilika ghafla

1. Nikisikia sijui uchaguzi natamani nizibe masikio

2. Nikisikia sijui fulani kala hela ya nchi natamani kutapika

3. Nikisikia katiba sijui miradi ambayo haijaisha miaka inaenda natamani kuhama hata nchi

4. Nikisikia bunge yaani huwa naona napoteza muda wangu kabisa kusikia chochote

5. Kitu pekee natamani kusikia ni ndoto za vijana wakijaribu kuinuka na kupambana kusapoti familia zao nk

6. Huwezi amini nimeanza kufatilia taratibu za kuomba uraia nchi Jirani. When I hear about Tanzania, am very much demotivated.

Jamani hii ni hali ya kawaida au ni ugonjwa fulani
 
Reactions: 30P
Ni ugonjwa unao, Unatakiwa kuipambania nchi yako kuliko kitu chochote, kazi ya kupambana na majangili ya CCM siyo ya kitoto.
 
Ni walele tu, kapita Punda kaingia N'gombe wote wala "MAJANI"!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…