Wakuu, tujaribu kuupitia utendaji wa Magufuli katika awamu ya nne na kwa kuanzia naanza na makala hii kutoka gazeti la Tanzania Daima
JANA vyombo vya habari nchini vimechapisha taarifa za ajabu. Taarifa hizi zinasema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Pombe Magufuli, ametishiwa kuuawa na waandishi wa habari.
Waandishi anaowatuhumu ni Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, John Bwire, Mhariri wa Rai, Muhingo Rweyemamu na mwandishi wa Rai, Neophitius Kyaruzi. Ametoa taarifa polisi Dodoma Julai, mwaka huu na kupewa RB namba DO/IR/3085/2006.
Katika mashitaka yake, anasema wahariri hao na mwandishi huyo wamemtishia kwa kutumia SMS kuwa watamuua.
Wao katika utetezi wanasema waliwasiliana naye kupata ufafanuzi juu ya taarifa za barabara ya Usagara hadi Geita, zilizoonyesha kuwa kuna mahali hakutenda kwa usahihi, hali iliyoitia serikali hasara.
Source: Tanzania Daima
Gazeti la Rai la Alhamisi [Oct 5 - Okt 11] limekuja na habari yenye kichwa hicho hapo juu.
Dondoo ni kuwa:
Wakala wa majengo, taasisi iliyo chini ya wizara ya Miundo mbinu, imemuuzia nyumba bwana Musa Joseph Magufuli (mdogo wake waziri Magufuli) huku akiwa na mkataba ambao unaonyesha angefanya kazi kwa miezi mitatu tu (26/09/2005 - 31/12/2005). Nyumba aliyouziwa iko ubungo, na ameuziwa kwa Tshs. 1.5M (!). Wakati anapewa ajira hiyo (Afisa tawala, business support unit), bwana Musa alikuwa na bado ni mwanafunzi wa masters UDSM. Alipoanza kazi tu akaanza kushughulikia ununuzi wa nyumba na within one month akawa na nyaraka zote muhimu za kumiliki nyumba hiyo. Wahadhiri wake UDSM wamesema kwa ratiba ya masomo yake ilivyokuwam masomo na kazi visingewezekana. Bwana Musa Magufuli aliacha kazi siku mbili kabla ya mkataba kwisha, akiwa na nyumba!
Mpo hapo? Sijui waziri atatuambiaje katika hili. Otherwise makeke yoote yale ya nyumba za NHC etc itakuwa anatuzuga tu.. nae yumo. ... labda aseme huyu ndugu alichakarika kivyake katika hili suala na yeye hakuhusika.
Mussa Magufuli ni mdogo wake na JP Magufuli ambaye aliuziwa nyumba ya serikali na kaka yake mwezi mmoja baada ya kumaliza chuo kikuu. Pia aliajiriwa na serikali akiwa bado hajahitimu chuo kikuu bila diploma wala certificate. Huyu ndio muadilifu mnayetaka apewe ikulu
Source: Gazeti Rai Novemba 7, 2008
Mussa Magufuli ni mdogo wake na JP Magufuli ambaye aliuziwa nyumba ya serikali na kaka yake mwezi mmoja baada ya kumaliza chuo kikuu. Pia aliajiriwa na serikali akiwa bado hajahitimu chuo kikuu bila diploma wala certificate. Huyu ndio muadilifu mnayetaka apewe ikulu
Source: Gazeti Rai Novemba 7, 2008
Unalipwa kiasi gani na lowasa umekurupuka huko kuja kupost pumba inamaana watu wote waliouziwa nyumba ni wadogo zake Mh rais magufuli au?
Za kuambiwa changanya na za kwako
tuache ushabiki maghufuli sio muadilifu kamwe. aliwahi kulazimisha barabara kuu ipite jimboni kwake kinyume na ramani ya barabara....