Monduli Vs Chato kimaendeleo kwa ujumla wake!

Monduli Vs Chato kimaendeleo kwa ujumla wake!

Mwanga Kilimanjaro ndio bora nchini mleta mada tunachagua rais wa nchi sio chato na munduli

Mwanga....pale mjini hata maji ya kunywa shida.....wakazi wa Mwanga maskini bado huwez linganisha na Vunjo wako juu sanaaa
 
Kafanya mambo makubwa saaana, yapi????? Taja kama kweli wajua!!!

Shule za monduli nyingi ni boarding kwasasa.....maji hasa monduli ya chini sio shida,,shule za msingi zipo za boarding pia......hospitali zipo za heshima......vituo vya afya ......vya hadhi....huyu mzee ni visionary leader
 
Chato ;

kuna mpaka taa za kuongozea magari

imekuwa wilaya 2000

hospitali ya chato ndo hosp kubwa kabla ya kuwa wilaya

kivuko

lami

generi ya kuchakachua pamba

wana ziwa victoria

wana raisi mtarajiwa

barabara za lami

umeme wa uhakika wa tanesco

shule za msingi 102

sekondari 45
 
Chato kuna taa za barabarani.. Kwi kwi kwi😂😂
 
Hawa wamasai wanaotangatanga na ngombe wao hawatoki monduli? Basi lowasa atakuwa mbinafsi sana.
 
Lowasa ameweka maji safi na salama toka mlima meru mpk wilayan kwake, huyu jamaa anachukia umaskin kweli
 
Asante sana mleta mada. Kwanza Monduli hakuna shule za kata, shule zote ni bweni, pili kuna hospitali kubwa, nzuri na huduma safi kuliko ya mkoa (mt. meru) , tatu barabara ni lami, nne ardhi ya monduli ni kame (hakuna mto wala ziwa wala bahari) ila ametoa maji Meru ambapo wanaoishi meru hawana maji ila monduli wana uhakika wa maji safi! mpo apo? LOWASSA ANATUFAA KWA KIZAZI HIKI NA KIJACHO!

BIG UP UKAWA KWA KUPATA JEMBE.!!!!!
 
Asante sana kwa mchango wako! Upi wito wako kwa Watanzania kwa ujumla?
 
Tunaomba wenyeji wa majimbo haya mawili watuambie ukifananisha majimbo haya mawili ni jimbo gani liko katika hali nzuri zaidi kimaendeleo?

Shida za wananchi ni nani anayezijua zaidi jimboni kwake? Vipi kwa muonekano wa hali za wananchi kiuchumi kwa ujumla wake pia?

Hebu tuangalie Elimu, afya, Umeme, maji, chakula, barabara nk.

Nimeuliza hili Swali kwa nia njema tu kwa sababu hawa waheshimiwa wagombea Urais wote wawili wamekua wabunge na Mawaziri muda mrefu!Je ni nani kati yao aliyezijua shida za wananchi mapema na akawasaidia kiukweli hasa?

Kama mtu amezifahamu shida za wananchi wa jimboni kwake mapema na akawaweka vizuri kimaendeleo basi huyu ndiye atakayewavusha watanzania wote na ndiye anazijua shida za wananchi wote.

Mleta mada una akili sana wewe........Lowasa hata Kinana alimsifiaga alipotembelea Monduli.
 
Kiukweli Lowassa amefanya yake kwenye Jimbo la Monduli.

1. Ni jimbo ambalo amehakikisha hakuna upinzani toka aingie madarakani.

2. Huduma za kijamii kama Hospital, Shule za msingi na Secondary, Maji Vyuo vya ualimu na Ufundi, pia alikua kwenye mkakati wa kuanzishwa kwa chuo kikuu, Yote haya yamefanyika chini ya uongozi wake.

3. Uanzishwaji wa shile za kata nchi nzima katika kipindi kifupi cha miaka 2 na kufanikiwa kwa zaidi ya 70% ni ushindi tosha.

Naamini Mungu akimjalia afya njema ataifanyia Tanzania makubwa zaidi na kuifanya Tanzania mpya.

Mungu Mbariki Lowassa awe na moyo wa hekima katika kuliongoza taifa hili katika Nchi ya Ahadi
 
Asante sana kwa mchango wako! Upi wito wako kwa Watanzania kwa ujumla?

Wito wangu ni kumchagua Lowassa kwa nia moja kwamba tutapiga teke umaskini ambao unatusakama hali tukiwa na rasilimali nyingi kuliko nchi yeyote ya Afrika Mashariki.
 
Wito wangu ni kumchagua Lowassa kwa nia moja kwamba tutapiga teke umaskini ambao unatusakama hali tukiwa na rasilimali nyingi kuliko nchi yeyote ya Afrika Mashariki.
Ok, asante a ubarikiwe!
 
Wito wangu ni kumchagua Lowassa kwa nia moja kwamba tutapiga teke umaskini ambao unatusakama hali tukiwa na rasilimali nyingi kuliko nchi yeyote ya Afrika Mashariki.
Ok, asante na ubarikiwe!
 
Mimi nimekaa Monduli kwa hiyo napafahamu kwa kiasi chake. Monduli ina shule za sekondari nyingi saana, za serikali lakini pia za binafsi kwa mfano Monduli mjini kuna shule mbili za serikali ambazo ni Irkisongo pamoja na Engutoto, shule hizi zote ni high schools, pia kuna shule za binafsi ambazo ni Moringe Sokoine pamoja na Maasai Girls, Maasai Girls watoto wanasoma bure, wanapewa kila kitu bure na wanasomeshwa mpaka watakapofika ukomo wao. Lakini pia kuna shule nyingine kama Moita Bwawani, Makuyuni na nyingine nyingi. Hiyo ni kwa upande wa shule za sekondari.
 
Lowasa atatuletea haya
 
Attachments

  • 1440244274256.jpg
    1440244274256.jpg
    50.9 KB · Views: 180
Chato kuna mpaka taa za kuongozea magari

Nonsense! Hizo taa zinaruhusu na kuzuia ng'ombe!

Hakuna kiasi hicho Chato, usilete data za kupewa, ishi mazingira halafu post hapa! Huu ni ufedhuli uliofanywa na Magufuli.
 
Back
Top Bottom