Monduli Vs Chato kimaendeleo kwa ujumla wake!

Monduli Vs Chato kimaendeleo kwa ujumla wake!

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Tunaomba wenyeji wa majimbo haya mawili watuambie ukifananisha majimbo haya mawili ni jimbo gani liko katika hali nzuri zaidi kimaendeleo?

Shida za wananchi ni nani anayezijua zaidi jimboni kwake? Vipi kwa muonekano wa hali za wananchi kiuchumi kwa ujumla wake pia?

Hebu tuangalie Elimu, afya, Umeme, maji, chakula, barabara nk.

Nimeuliza hili Swali kwa nia njema tu kwa sababu hawa waheshimiwa wagombea Urais wote wawili wamekua wabunge na Mawaziri muda mrefu!Je ni nani kati yao aliyezijua shida za wananchi mapema na akawasaidia kiukweli hasa?

Kama mtu amezifahamu shida za wananchi wa jimboni kwake mapema na akawaweka vizuri kimaendeleo basi huyu ndiye atakayewavusha watanzania wote na ndiye anazijua shida za wananchi wote.
 
Huwez ...linganisha jimbo la lowasa liko juu...kwake hata wapinzni ni kama hawapo .....alikuwa anawajali wananchi wake kila wakati....Makufuli....ziwa victoria lile ila no maji......
 
Huwez ...linganisha jimbo la lowasa liko juu...kwake hata wapinzni ni kama hawapo .....alikuwa anawajali wananchi wake kila wakati....Makufuli....ziwa victoria lile ila no maji......
So hapa unatoa taswira gani mkuu?
 
Mkuu kumlinganisha lowasa na makufuli ni kumdhalilisha lowasa ....Monduli japo wakaze wake wengi ni wafugaji na wakulima ila lowasa kafanya mambo makubwa sanaaa
Aisee!Unatoa wito gani kwa watanzania kwa ujumla?
 
Tunaomba wenyeji wa majimbo haya mawili watuambie ukifananisha majimbo haya mawili ni jimbo gani liko katika hali nzuri zaidi kimaendeleo? Shida za wananchi ni nani anayezijua zaidi jimboni kwake? Vipi kwa muonekano wa hali za wananchi kiuchumi kwa ujumla wake pia?
Hebu tuangalie Elimu, afya,Umeme,maji,chakula,barabara nk.
Nimeuliza hili Swali kwa nia njema tu kwa sababu hawa waheshimiwa wagombea Urais wote wawili wamekua wabunge na Mawaziri muda mrefu!Je ni nani kati yao aliyezijua shida za wananchi mapema na akawasaidia kiukweli hasa? Kama mtu amezifahamu shida za wananchi wa jimboni kwake mapema na akawaweka vizuri kimaendeleo basi huyu ndiye atakayewavusha watanzania wote na ndiye anazijua shida za wananchi wote.

Lowassa ndiye aliezifahamu matatizo ya wananchi wake na akachukua hatua. Baada ya kuwa mbunge 1995 aligundua tatizo ni elimu na akachukua hatua, wakati anakuwa mbunge, jimbo lake lilikuwa na shule moja ya sekondari na mwamko wa elimu ulikuwa mdogo. Lowassa anaacha ubunge 2015, Jimbo lake lina shule za kutosha hadi kuna kata zina shule mbili na zina ubora. Ni mafanikio makubwa kwa jamii ya wafugaji. Mwamko wa elimu kwa wafugaji wa Monduli ni mkubwa kuliko pengine.Kuna vijana wengi wa Monduli wenye elimu ya juu kuliko pengine. So Lowasa anastahili kuwa rahisi.
 
moduli wana hosp kubwa sana kama ya mkoa.
 
Asante kwa mchango wako mkuu!Na wewe unawaambia nini watanzania kwa ujumla?
 
Mwanga Kilimanjaro ndio bora nchini mleta mada tunachagua rais wa nchi sio chato na munduli
 
Binafsi monduli kuna shule za msingi za boarding...za serekali ...sijui chato zinapatikana kwel....???
 
Zaidi ya 87% ya shule za secondary kwenye kila kijiji ni shule za bweni, zaidi ya 70% ya Barabara ni lami
 
Huwez ...linganisha jimbo la lowasa liko juu...kwake hata wapinzni ni kama hawapo .....alikuwa anawajali wananchi wake kila wakati....Makufuli....ziwa victoria lile ila no maji......

anachokijua makufuli ni mijisifa ya kukariri takwimu za serikali tu!
 
Mkuu kumlinganisha lowasa na makufuli ni kumdhalilisha lowasa ....Monduli japo wakaze wake wengi ni wafugaji na wakulima ila lowasa kafanya mambo makubwa sanaaa

Kafanya mambo makubwa saaana, yapi????? Taja kama kweli wajua!!!
 
Monduli pako vizuri, jamaa kupambana sana kwenye lile jimbo
 
Back
Top Bottom