Escrowseal1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 4,600
- 4,576
Salamu Kwa wanajamii wote humu ndani. Nimekutana mkasa mmoja ulinigusa Sana ukiwa ni matokeo Ya wafanyakazi hewa.kijana mmoja mwalimu alikuwa masomoni akichukua degree Ya ualimu akitokea kazini inasemekana katika kuhakiki hilo zoezi waliambiwa kuhakiki kwa waajiri wao kama wanasomea Ama wanajiendeleza katika Nafasi zao wanazotumikia tatizo ni pale hakupata taarifa Ya uwasilishaji matokeo yao ama nyaraka na alivyoshtuka na kukimbia huko lindi akajikuta hawezi kupata msaada toka kwa mwajiri kwa Kuwa ameshafukuzwa kazi.mbaya zaidi mwajiri anamwambia hakuna msaada wowote anaoweza kupatiwa.
Naamini nia Ya Raisi ni njema Kabisa na sidhani kama alilenga vijana kama hao wanaopambana kujikwamua kimaisha. Wote tunajua hali ilivyo kutoka katika mazingira yetu. Mtu kujiendeleza toka diploma Hadi degree bado ni Faida kwa Taifa.kuna baadhi Ya waajiri watatumia loop hole kukomoana hasa katika fani hii na wengi wanajua jinsi sector yetu hii waajiri wengi walivyo hasa likija suala hili kupewa ruhusa Ya kusoma nk. Sasa ni vema pia madhara Ya hii operation yafanyiwe kazi na wahusika. Mtu anaelitumikia Taifa na akafanikiwa kujipatia nafasi Ya kujiendeleza kufukuzwa katika mwaka wa mwisho wa masomo yake si tu kuharibia maisha bali Pia ni hasara kwa Taifa letu ukizingatia anafanya kazi remote areas ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii.
Mh Raisi anafanya right thing kuondoa watu hewa lakini kweli watu kama hawa nao ni hewa? waajiri nao wawe reasonable ku solve matatizo yanayotokana na operation hii na wasifanye kazi kwa uoga na kuharibiana. Siamini kama Mfano wa huyu kijana hakukuwa na immediate head ama headmaster ambaye angeshindwa kuhakikisha anapata communication ili kuokoa maisha yake ili asiishie kufukuzwa ni dhahri sekta Ya ualimu Ina mahead wanoko wengi hasa mtu anapojiendeleza huwa wengi hawafurahii na madhara haya yanaweza Kuwa ni matokeo yake Kwani wengi waliotoka huko kwenda chuo huwa wanakumbana na changamoto nyingi sana kwani wengi wa wakubwa zao hawapendi.
Naamini mh Raisi ana nia njema sana tu na siamini kama anaweza kufurahia mkasa kama huu kama kweli waajiri wanaweza ku report matokeo hasi wanayokumbana nayo. Naamini siyo offence kufanyia marekebisho issue kama hizi kwani wote ni binadamu na hatuwezi fanya kazi kama malaika. Sioni kwa nini mwajiri wake asimsaidie kufuata channel kwani kumwacha mtaani si tu kumharibia bali kuingiza hasara kwa Taifa kwani amesomeshwa miaka mingi sana na afukuzwe tu kwa kutokujua kama alitakiwa kuwasilisha nyaraka. Inawezekana wapo na wengine basi mamlaka zifanye kazi zake reasonably bila kukomoana. Hata Baba wa Taifa aligundua madhara Ya operation vijiji na hakusita kukiri mapungufu.