MOI mnataka tushindwe kumlipia ndugu yetu gharama za matibabu?

D2050

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
1,902
1,067
Ndugu alipatwa na ajali ya pikipiki mwezi wa 11 2019 maeneo ya Gongo la Mboto, alipelekwa hospitali ya Amana napo wakashauri apelekwe MOI.

Baada ya kumpeleka MOI toka tarehe 18/11/2019 hadi leo mgonjwa hajatibiwa mnataka afe? Muda aliokaa kitandani hapo bili mtakayoleta hapo baadae mnataka tushindwe kulipa?

Waziri wa Afya na Mkuu wa Kitengo cha MOI wagonjwa wengi wanalalamika kutopata huduma zilizo sahihi na kwa wakati. Kumbukeni hao wanaoumwa hawakutaka kuumwa bali mwenyezi Mungu ndio kawapangia.

Manesi wa MOI wana kauli za hovyo hawapendi kuwasikiliza wagonjwa hadi uwape rushwa ndio mgonjwa wako atasikilizwa.
 
Sababu wanazotoa kwanini hatibiwi ni zipi?
Bima? Madaktari hawatoshi? au ni Uzembe

By the way sababu yoyote kati ya hizo pia kwangu mimi ni uzembe, hata kutomtibu mtu kwa kukosa Bima kwenye nchi kama ya Tanzania ni mauaji
 
D2050,
Kaumia nini?
Labda kavunjika mfupa anahitaji operation?
je amekuta wenzake wangapi wapo kwenye foleni ya kusubiri operation?
Au kaumia kichwa labda so matibabu wanayompa ni uangalizi wa karibu ila ahitaji operation
labda ungefafanua zaidi wadau wangeweza kushauri
 
Angempeleka mtoto hospital ya wilaya tu, Muhimbili ni hospitali ya matajiri ile
Labda walimhamishia kwenda muhimbili kwa huduma zaidi. Kama alilazwa ICU hizo ndo gharama zake. Watu wanauza magari etc kulipia matibabu mtu akilazwa ICU. Hapo ndo kama una bima unaenda kanisani au msikitini kutoa sadaka ya shukrani. Medical care ni gharama sana. Ukiongea na watu waliofeli figo wanafanya dialysis sijui ndo utaona gharama balaa. Au matibabu ya kansa kama unajilipa ni balaa jingine
 
Back
Top Bottom