Serikali Mkoani Iringa imeifungia na kuinyanganya kampuni maarufu ya Mohammed Enterprise kufanya biashara ya mbolea mkoani Iringa. Sababu kuu ya serikali ya mkoa kuchukua hatua hiyo dhini ya kampuni ya Mohammed Enterprise ni baada ya kukuta mbolea ktk maghala ya kampuni hiyo ikiwa:
Haina viwango vya ubora
Mbolea imeganda
mifuko haionyeshi expiry date
mifuko haina viashiria vya mchanganyiko wa mbolea
Wakulima mkoani Iringa wameelezea wasiwasi wao wa kupata mazao bora baada ya pembejeo hiyo toka Mohammed Enterprise kukosa viwango na kurudisha nyuma juhudi za kauli-mbiu KILIMO KWANZA.
Kampuni ya Mohammed Enterprise imeshaandikiwa barua kuhusu hatua hiyo na viongozi wa Mohammed Enterprise wamekubali hatua hiyo ya serikali.
Ipelekwe maabara kabisa kuchunguza ni mchanganyiko wa aina gani kwani hata kuimwaga au uteketezaji wake unaweza leta madhara.Iko kiasi gani na ilipitishwa na mamlaka ipi ya viwango. Wakuwajibika hapo sio MeTL peke yao.