Mohamed Banka, Mussa Hassan Mgosi ,Teja Chuji out Simba SCC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mohamed Banka, Mussa Hassan Mgosi ,Teja Chuji out Simba SCC

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, Jul 14, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 99%, align: left"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody"]HALI ndani ya klabu ya Simba sasa imekuwa ya mtafutano, baada ya wachezaji Mussa Mgosi na Mohammed Banka kuenguliwa kwenye usajili kwa ajili ya Ligi Kuu msimu ujao.

  Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Simba kufungwa na Yanga bao 1-0 katika mchezo wa fainali ya Kombe la Kagame uliofanyika Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Habari za kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Simba zilieleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika hoteli moja maarufu jijini Dar es Salaam, ambapo pia walikubaliana kuachana na kiungo mpya Athumani Idd ‘Chuji’.

  “Kikao kimekubaliana Banka, Mgosi na Chuji wasiwepo kwenye kikosi chetu kitakachoshiriki Ligi Kuu msimu ujao, hivyo tuachane nao. “Nia ni kujenga timu yenye wachezaji wenye viwango na damu changa kwa nia ya kuwa na kikosi cha ushindani,” alisema mtoa habari wetu.

  Hata hivyo chanzo hicho kilieleza kuwa suala la Mgosi lilizua mjadala mrefu kwenye kikao hicho na wakakubaliana kuwa mchezaji huyo kwa vile anatakiwa na timu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni wakati mwafaka wa kumruhusu aende.

  “Kwa hiyo Mgosi ameachwa kwa sababu anatakiwa Motema Pembe, lakini Banka na Chuji viwango vyao havikumridhisha kocha Mosses Basena,” kilieleza chanzo hicho ambacho hakikutaka jina lake litajwe gazetini.

  Mtoa habari huyo alieleza kuwa Simba pia imeamua kuachana na Mgosi baada ya mshambuliaji wake Emmanuel Okwi aliyekuwa ameenda Afrika Kusini kwa majaribio na timu ya Kaizer Chiefs kutofanikiwa hivyo atarejea kuichezea timu hiyo.

  Mgosi na Banka walikuwepo kwenye kikosi cha Simba kilichoshiriki Ligi Kuu msimu uliopita, wakati Chuji alirejea Simba Juni mwaka huu akitokea Yanga ambayo alimaliza nayo mkataba tangu Aprili mwaka huu.

  Chuji alijiunga Yanga mwishoni mwa mwaka 2006 akitokea Simba ambayo alijiunga nayo mwishoni mwa mwaka 2005 akitokea Polisi Dodoma.

  Alipoulizwa jana kuhusiana na habari hizo, Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage alisema yupo nje ya Dar es Salaam ingawa alikiri kuwepo kikao cha Kamati ya Utendaji juzi.

  “Sijapata taarifa hizo, labda nizifanyie kazi kwa sasa, maana nipo nje ya Dar es Salaam,” alisema Rage.

  Lakini suala la kuachana na Mgosi na Banka linaweza kuwasumbua Simba kutokana na muda wa kuacha wachezaji kuwa tayari umepita.

  Kipindi cha kutangaza wachezaji ambao timu zinawaacha kilikuwa kati ya Juni 1 hadi Juni 20 mwaka huu, ambapo hivi sasa ni kipindi cha uhamisho ambacho kitamalizika kesho na muda wa mwisho wa usajili itakuwa Julai 20 mwaka huu.

  Wakati huohuo, kiungo wa Simba Jerry Santo yupo mbioni kujiunga na timu ya Hoang Anh Gia Lai ya Vietnam.

  Klabu hiyo ambayo anachezea Mkenya mwingine Allan Wanga imekuwa ikifanya mipango ya kumsajili kiungo na kuwa taratibu za kusafiri kwenda Vietnam kwa mipango zaidi wiki hii inafanyika.

  Chanzo cha habari kiliueleza mtandao wa SuperSport.com kuwa hivi sasa Santo anafanya taratibu za viza kwenda nchini humo kukamilisha mipango ya kujiunga na timu hiyo. Santo amebakisha miezi mitatu katika mkataba wake wa kuichezea Simba ya Tanzania.

  Mtandao huo umeeleza kuwa timu hiyo imevutiwa na Santo na kuwa kitakachobaki ni kama ataafikiana na suala la maslahi au la.

  Santo alitoa mchango mkubwa kuiwezesha Simba kufika fainali ya michuano ya Kombe la Kagame, ingawa alishindwa kucheza Jumapili mchezo wa fainali kutokana na kuwa na adhabu.

  Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alipoulizwa jana kuhusiana na habari hizo za Santo, alisema bado hajapata, lakini anachofahamu ni kuwa Santo amebakisha mkataba wa miezi mitatu kuchezea Simba.

  “Inawezekana anaangalia maslahi, lakini ninachojua bado ana mkataba wa miezi mitatu,” alisema.

  Kuhusiana na suala la Okwi alikiri mchezaji huyo kutomalizana na Kaizer Chiefs na kuwa ataendelea kuchezea Simba msimu ujao na kwamba hivi sasa ameenda kwao Uganda.

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: Text"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Soka la Bongo bwana uzushi mtupu
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Simba bana wakiukalia hawaishi kutafuta visingizio kibao
   
 4. papason

  papason JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Rage ni kiongozi dhaifu mwenye uwezo mdogo kiutendaji, domo kwa sanaa, na mpenda kuendekeza migogoro na mifarakano kwenye kila tasisi anayoingoza tena wanasimba msipo mshitukia mapema atawapeleka pabaya mwishoni awaache kwenye mataa! waulizeni Tabora, Saigon, DRFA, FAT
   
 5. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Watanzania tubadilike, tusitapetape na kuwaponza walioipigania timu mpaka kufika fainali KISHA WATOLEWE KAFARA.
  Viongozi wa soka acheni ubabaishaji katika hilo.
   
 6. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kwenye kombe la hisani august mwaka huu simba ikifungwa tena sijui watamfukuza nani siku hiyo. au watavunja kikosi? Bongo bwana
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,246
  Likes Received: 5,627
  Trophy Points: 280
  sasa wametagaza kumuondoa bwana wao mgosi unafikiri watafungia wapi tena
   
 8. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  Wanatafuta pa kutokea hao viongozi wababaishaji baada ya kupakatwa.
   
 9. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 849
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Hapo kwenye red sijapaelewa! Yaani kiwango kimeshuka halafu anazwa????!!!!
   
 10. M

  Masuke JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mbona habari za kusajiliwa Felix Sunzu hawajaandika?
   
 11. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kufukuzana ndo msingi wa maendeleo ya soka la bongo, akiondoka atafunga mwingine. Tangu mwaka 1936 wamekuja na kuondoka wafungaji kibao japo si vizuri kufukuzana kila timu inapoharibikiwa.
   
Loading...