Moderm nzuri kuliko zote ni ipi?tigo,airtel?voda?zantel?ttcl? what is the best?

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,537
6,458
waheshimiwa, tafadhali, naombeni mwenye uzoefu wa hizi moderm za internet za mitandao ya simu anisaidie kitu hiki, mwanzoni nimekuwa nikitumia zantel kwa muda mrefu, nilikuwa Dar es salaam, niliposafiri kuja mkoani kwa kuhamishwa kikazi, haipatikani hata ukisimama kwenye kilima kirefu namna gani...nimeiweka sandukuni hadi nikitembelea dar. nilikuwa naona kama wao, hasa kwa dar ndo wazuri kwahabari ya bei nafuu, hasa hybrid, bundle zao za wiki na mwezi.

sasa huku mkoani nataka kupata net mpya,...matangazo kwenye radio na tv ni mengi, kila mtu anashindana hata hawahawa zantel ambao mkoani hawapo...naombeni mzoefu anisaidie, mtandao gani bora kuliko yote, wenye bei nafuu kwa mtu wa kipato cha chini, ulio faster na unaofika Tanzania nzima kwa internet? nitashukuru sana kama mtanisaidia jibu...kati ya hiyo niliyoiweka juu.
 
Mi ningependa kujua upo mkoa upi hasa lakini nijuavyo modem ya voda ndiyo safi nimekuwa nikitumia mkoa wa kilimanjaro.
 
niko singida, zantel haishiki kabisa hata ukipanda juu ya kilima...voda naogopa garama, kati ya tigo na airtel ipi bora kwa garama na speed kubwa?thanks all for ur contributions.
 
kwa uzoefu wangu i think tigo ni nzuri kwani unaweza kuchakachua extreme kwa mia 350 tu siku nzima speed ya farasi
 
modem ya airtel ni nzuri na inafaa kwa mtanzania wa kipato cha chini kwaupande mwingine network ya Airtel imesambaa nchi nzima.
 
Tumia Airtel ndio ipo poa hata coverage yake ni kubwa lakini Zantel hamna kitu mimi mwenyewe modem yangu ya Zantel nimeweka sandukuni.
 
niko singida, zantel haishiki kabisa hata ukipanda juu ya kilima...voda naogopa garama, kati ya tigo na airtel ipi bora kwa garama na speed kubwa?thanks all for ur contributions.
Mkuu kama upo huko basi nunua modem ya Tigo kisha ichakachue uitumie kwa voda na airtel maana ni bei rahisi,
Pia waweza nunua ya voda ukaichakachua pia ili uweze kuitumia kwa Tigo na aitel ila bei ipo juu,
Sikushauri ya airtel ngumu kuchakachulika unless kama umepanga kutumia kwa airtel tu
 
modem Safaricom upto 7.2Mbps,mtandao Airtel au Vodacom.........
 
Attachments

  • IMG_0039[1].JPG
    IMG_0039[1].JPG
    179.9 KB · Views: 111
waheshimiwa, tafadhali, naombeni mwenye uzoefu wa hizi moderm za internet za mitandao ya simu anisaidie kitu hiki, mwanzoni nimekuwa nikitumia zantel kwa muda mrefu, nilikuwa Dar es salaam, niliposafiri kuja mkoani kwa kuhamishwa kikazi, haipatikani hata ukisimama kwenye kilima kirefu namna gani...nimeiweka sandukuni hadi nikitembelea dar. nilikuwa naona kama wao, hasa kwa dar ndo wazuri kwahabari ya bei nafuu, hasa hybrid, bundle zao za wiki na mwezi.

sasa huku mkoani nataka kupata net mpya,...matangazo kwenye radio na tv ni mengi, kila mtu anashindana hata hawahawa zantel ambao mkoani hawapo...naombeni mzoefu anisaidie, mtandao gani bora kuliko yote, wenye bei nafuu kwa mtu wa kipato cha chini, ulio faster na unaofika Tanzania nzima kwa internet? nitashukuru sana kama mtanisaidia jibu...kati ya hiyo niliyoiweka juu.

ZANTEL ni bomba kinoma
 
Hakuna mtandao ambao unazidi mitandao yote kwa kila kitu. HAKUNA. Narudia, Hakuna mtandao ambao unazidi mitandao yote kwa kila kitu. HAKUNA. Ubora wa mtandao hutegemea na gharama ya awali ya kununulia, gharama wakati wa matumizi baada ya kununua, signal strength n.k. Mtandao unaweza kuwa na gharama nzuri lakini usimfae mtu heavy user kwa sababu ya weak signal strength. Mtandao unaweza kuwa na signal strength kubwa na gharama nafuu lakini hauna coverage kubwa hivyo si kila mtu wa kila mahali atauhitaji.

Fanya utafiti, fahamu coverage na strength. Nilikuwa na sasatel, wakaniboa gharama (enzi hizo MB 400 or 600?) ilikuwa ni 30,000/=. Nikachukua Zantel (120,000/=) Nikajiunga package ya highlife. Zantel spidi safi, nikaenjoy. Wakaja na sera huwezi kurecharge hadi 7 days za highlife zifike, nikavumilia. Wakaja na sera huwezi kurecharge highlife package hata kama 7 days zimefika hadi uwe umepiga simu for not less than 5,000/= per week. Uvumilivu ukanishinda. Nikanunua Airtel 60,000/=. Nilipokuwa naishi (segerea) spidi ndogo kweli. Nikienda town (posta) spidi ya ndege, safi. Nikirudi nyumbani maumivu. Nikarudi tena sasatel. Kwa sasa wakawa wanauza modem kwa 39,900/=. Wana package ya 1.5 GB kwa 7500/= for one week. Spidi ya kusuasua, wakati mwingine kasi. Nikahama makazi kwenda sehemu nyingine hapa Dar (kinyerezi). Sasatel, spidi ya kobe. Nikajarudia modem yangu ya Airtel niliyoiweka kapuni. Spidi kubwa. Ndo nayotumia sasa. Wana packages kadhaa, nazotumia 3GB/week/15,000/= na 400MB/Month/2500/=. Unarecharge hata kama umemaliza package yako hapo hapo, no "hadi wiki iishe" kind of limitations.

Hivyo fanya research. Majibu mepesi ya Tigo, Voda, Airtel, Zantel, TTCL, Safaricom yatakuchanganya tu. Isitoshe spidi za modems kama 3.1 Mbps, 7 Mbps etc ni uwezo wa modem na si mtandao. Gari lenye kasi haliwezi kwenda maximum speed kama barabara ni mbovu au kuna foleni. Simply like that.

Kama unapenda kudanganywa, sawa.
 
Back
Top Bottom