Maji Maji Maji Jinsi Yanavyo Sababisha Simu/Computer Kufa au Kuharibika.
Maji ni uhai, kila mtu anajua hilo. Na maji yamekuwa kimiminika muhimu sana kwenye maisha yetu, tunayanywa, tunayaoga, tunapozea mitambo n.k
Maji hayohayo yakienda kusiko yanaleta uharibifu mkubwa. Anyway mimi ni fundi simu, computer, Tv na Music System kwa hiyo nisiwachoshe na stori ndefu.
LEO TUZUNGUMZIE MAJI KWENYE SIMU.
Kwa uzoefu wangu wa muda mrefu kwenye ufundi wa vifaa tajwa, maji yanaongoza kuua au kuleta uharibifu kwenye sakiti za vitu hivyo.
Wote tunajua kuwa maji ni kipitisha kizuri cha umeme, pia maji yakiungana na chuma na hewa yanazaa kitu kinaitwa Ferric Oxide (kutu) kwa hiyo;
1. Maji yanapitisha umeme
2. Maji+Chuma(Fe)+Oxygen (O2)=Ferric Oxide (2Fe2O3.XH2O(s) (kutu)
Vitu hivyo viwili vinaharibu simu, maji yatapigisha shot sakiti (short circuit) kwa sababu yanapitisha umeme na kuunga njia za umeme ambazo hazipaswi kuungana.
Ferric Oxide (kutu) itasababisha vitu vyenye uchuma (Fe) kulika.
Ushauri Wangu Simu Ikiingia Maji.
1. Zima simu mara moja, kama battery la kutoka toa battery. Hii itasaidia kupunguza flow ya umeme kwenye njia ambazo sio.
2. Kwa maji yanayoonekana nje, futa kwa kitambaa safi.
3. Peleka simu yako kwa fundi mzuri aliye jirani nawe, kama humjui wasiliana nasi, tutakuunganisha naye ili aikaushe maji.
4. Usishawishike kuiwasha na kuitumia kwa sababu tu inawaka. Usippziba ufa utajenga ukuta.
Kuna zile simu ambazo zina water [emoji97] resistance, ni nzuri ila kuwa na uhakika na kitu kimoja, simu yako ni factory [emoji555] sealed, kama ni hizi "refurbished" utalia ndugu yangu. Na ninashauri usijaribu simu yako ilowe kwa bahati mbaya tu.
Hapa Chini ni Samsung A52 iliingiwa na maji na ikawa inashindwa kuchaji. Simu imefika ofisini kwetu na tumeiweka sawa.
Kama unatatizo kama hilo, tupo kwa ajili ya kukupa ushauri mzuri zaidi juu ya kutatua tatizo kwa namna bora.
Sisi Tupo;
Barabara ya Juakali, Mwanjelwa
Mbeya
0767379327
Na mtandaoni tuko kila sehemu ya Tanzania, fuata kiungo hiki kuwasiliana nasi moja kwa moja kwa kujaza fomu mtandaoni [emoji116]
View attachment 2542097
View attachment 2542101