Nina-asume unazungumzia hiyo SMS Salama. Ungejaribu kujisumbua kidogo kusoma ile page pengine ingekusaidia kupata uelewa wa jinsi inavyofanya kazi, na ungeweza kujenga hoja ambayo ni relevant zaidi kwa manufaa ya wote.
Labda kwa marejeo tu, hiyo SMS Salama ina-encrypt message inapotoka kwenye simu yako ili uwe na uhakika kwamba huko itakapopita hakuna mtu anaweza kuisome. Kwa hiyo lengo lake sio kulinda SMS messages zilizo kwenye simu yako, kama ambavyo wewe umeelewa. Lengo lake ni kulinda messages pale zinapokuwa njiani kuelekea ulikozituma. Bila hivyo, kufuta messages hakusaidii kwa sababu inawezekana kupata message zote alizotuma na kutumiwa mtu kutoka kwa mobile operator hata kama amezifuta kwenye simu yake, na watu wanafanyaga hivyo mkuu.