Mob Justice

Hiyo sio mob justice ni mob injustice.Sio siri,ama kwa kujua au kwa kutojua,Watanzania wengi sana wameisha shiriki dhambi ambayo kwa dini yetu haina msamaha,dhambi ya kuua,wengi wana damu za binadamu wenzao mikononi mwao,hata watoto wadogo nao wanashiriki kwenye hii mob injustice,hii dhambi wanakua nayo na wengine wanasahau kuwa waliwahi kushiriki mauaji wakiwa wadogo na wengine dhambi hii uwatafuna ukubwani,Mungu epusha kizazi hiki na mob injustice
 
Sasa pengine hata ushahidi wa kuiba hako kakuku haupo... ila ushahidi wa mabilioni ya eskrow upo na wutuhumiwa wanatanua na kuabudiwa mitaani wakikingiwa kifua 'kutohojiwa' this is pure injustice.
 
Na asie na dhambi awe wa kwanza kumtupia jiwe!!

Mtu mmoja manzese alisikia kelele za mwizi akakimbilia akakutana na yule kibaka na kibaka kamgeuzia kibao na kumwita yeye ndiye mwizi akaanza kumpiga. Watu kuja bila kujua kibaka ni nani wakaanza kumpiga na kibaka akatokomea. Damu ya mtu asiye na hatia ikamwagwa.

Usihukumu nawe hautahukumiwa.
 

Ni mbaya saan mbaya saana! This should stop! LHRC mko wapi kwa hili?
 
Wote kwenye picha wanaotoa 'adhabu' kwa huyo 'mkosaji' wanaamini kwamba wafanyalo ni sawa na huyo 'mkosaji' anastahili hiyo adhabu. To them, they are 'justified' in their action.Ndio maana mleta mada kaweka concept ya justice - mob justice, not injustice! Ukizungumza na yeyote kwenye hilo kundi atakuambia: "Hii ndio dawa ya hawa vibaka bwana!"Hilo kundi linajiona linafanya kitu cha maana sana 'kukomesha' wizi au tabia mbaya. Ukiwaambia kwa nini msifanye hivyo kwa wezi wa mabilioni ya fedha, wanaguna na kusepa!
 
Ukiona hivi, pita uendelee na habari zako wala usijaribu kuwaambia kitu chochote hawa watu, watakuua na wewe.
 
Naona kijana wa CHADEMA amebeba tofali kwenda kumalizia kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…