Mo & METL out, tuachie Simba yetu

Abeltrainer

Senior Member
May 24, 2013
198
349
Wadau na wapenzi wa simba sport club naomba tuungane, katika kampeni hii ya kumshinikiza mo na kampuni yao ya METL kuondoka Simba, ili kupisha wawekezaji wengine.

Ni ukweli usiopingika kwamba uwekezaji wa mo na kampuni yao ya metl katika club yetu pendwa simba sport club hauna tija, hauna faida kwa simba na pia haueleweki
Tunahitaji kuwa wawekezaji wengi, ili

1. Kuwa na mtaji mkubwa,
2. Kuleta uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa timu kwa sababu viongozi hawatakuwa vibaraka mwekezaji

Tunataka wawekezaji watakao weka hela mezani na sio kwenda kununua bond bot halafu ile fida ndio uilete kuendeshea timu, huu ni uwekezaji ambao hauna tija.

Muwekezaji akitumia brand ya simba kwenye bidhaa zake anatakiwa kulipia, na ashindanishwe na makampuni mengine, kama akikosa basi.

Nawasilisha
 
Simba inachohitaji ni uongozi bora na kuwa ondosha kabisa hawa wana siasa akina Mangungu na Try again na wapuuzi wengine waliojazana mle ndani, Mo akiachia timu utaweza kuiendesha? au una wawekezaji wakuchukua nafasi ya Mo? kama hauna endelea kula ugali utulie
 
Sidhani kama shida ni MO, Nadhani ni nmna usajili wa simba ulivyo na mgao wa madaraka kwa mujibu wa katiba na miongozo ya simba. Kuna ngazi nyingi za maamuzi yanayotoa mianya mingi kuidhibiti timu. Hata ungekuwa MO, kwa usajili wa Simba ulivyo autonomy ya timu ndogo kwa MO. Watu wanatumia mianya hiyo kula hela. Tofauyi sana na Yanga Muundo wake umenyoka.
 
Kuna timu zimewekeza mahela mengi kushinda simba lakn hazina hata uwezo wa kufika robo fainali.... kikubwa hapa ni kukaa chini na kuangalia tatizo liko wapi na turekebishe.... mo huyu unae msema ndie aliyeleta chachu ya mabadiliko ya soka hapa TZ mpaka unavyoona simba na Yanga wamefika hapo walipo ni Ujasiri wa MO wa kuibadilisha Simba na iwe timu yenye ushindani. ko tupunguze zihaka kwa MO... tujaribu kuheshimu pia alichokifanya kwa soka la Tanzania
 
Simba ni Timu ya Mo, juz tu apa aliulizwa kitu gani aliwah nunua bei ghali akasema Simba na aliinunua miaka mitano ilopita, ukisema aondoke ataondoka na timu yake mzee. Mkuu unamfukuzaje owner ? . The Glazer family Owns man united kama majority shareholder huku Jim akiwa significant minority shareholder sasa Man u fans hawaitaki hiyo famili ya Glazer ila hawana la kufanya..
 
Miaka ile ya mabadiliko msisistizo wetu mkubwa ulikuwa.

1. Uwekezaji bora

2. Uongozi bora.

3. Wachezaji Bora.
Je tumepata uwekezaji bora?
Je tumepata uongozi bora?
Jibu HAPANA
Kwa nini
1.aina ya uwekezaji uliokuwa unahubiriwa hauna tija kwa upande timu,un tija upande wa muwekezaji tu, lwa sababu kwa uhakisia mo na kampuni yao hawajawekeza chochote simba, walichofanya ni kununua bond za 20billion, faida inayoptaikana ndio wanaileta simba..ina maana siku wakivurugana na simba, wanachukua 20billion yao
2.hamna ushindani kwani muwekezaji ni mmoja tu
3. Muwelezaji ndie aliyekuwa anaendesha mchakato mzima wa mabadiliko,kwa hiyo simba sport club ikakosa nguvu kimaamuzi,ndio maana mwenyekiti mkwabi alijiuzulu
4. Hatuna namna ya kumbana muwekezaji,ukiangalia mambo aliyoyaahidi hajtekeleza hata moja
Aliahidi
1.uwanja,
2. Academy
3.modern equipements kama gym,nk
4.modern hostel za wachezaji
5. Na mengine mengi
Hajatekeleza hata moja, labda tu ni kuuta ule uwanja wa uongo na kweli mo sport arena,na kiwazawadia wachezaji pikipiki za boxer, what a shame
 
Simba inachohitaji ni uongozi bora na kuwa ondosha kabisa hawa wana siasa akina Mangungu na Try again na wapuuzi wengine waliojazana mle ndani, Mo akiachia timu utaweza kuiendesha? au una wawekezaji wakuchukua nafasi ya Mo? kama hauna endelea kula ugali utulie
Hao watu wamewekwa na nani?
Hivi kati ya try again na mangungu ni nani alitakiwa awe raisi wa club?
 
Sasa nitawelaje hiyo elfu kumi kwenye timu ilihali mfumo ni mbovu, kwa nini hisa zisiuzwe kwa wanachama ili mwenye nayo anunue?
Kwa nini auziwe muwekezaji mmoja?
Umeandika kitu ambacho hauna uelewa nacho, hujui undani wa hili sakata, fatilia vyanzo mbalimbali usome na uelewe,

Kiufupi umekurupuka kwa mihemko, au itakua umesikia sehemu ukaamka nalo juu juu bila uelewa.
 
Kuna timu zimewekeza mahela mengi kushinda simba lakn hazina hata uwezo wa kufika robo fainali.... kikubwa hapa ni kukaa chini na kuangalia tatizo liko wapi na turekebishe.... mo huyu unae msema ndie aliyeleta chachu ya mabadiliko ya soka hapa TZ mpaka unavyoona simba na Yanga wamefika hapo walipo ni Ujasiri wa MO wa kuibadilisha Simba na iwe timu yenye ushindani. ko tupunguze zihaka kwa MO... tujaribu kuheshimu pia alichokifanya kwa soka la Tanzania
Hapana walikuwepo akina manji na nk
Cha msingi ni tuwe na uwekezaji wenhe tija, mo anasema ameinunua timu, alitoa kiasi gani, kimefanya nini?
 
Umeandika kitu ambacho hauna uelewa nacho, hujui undani wa hili sakata, fatilia vyanzo mbalimbali usome na uelewe,

Kiufupi umekurupuka kwa mihemko, au itakua umesikia sehemu ukaamka nalo juu juu bila uelewa.
Wewe ndio huelewi.. ebu nipe structure ya uwekezaji wa mo simba ilivyo
 
Simba ni Timu ya Mo, juz tu apa aliulizwa kitu gani aliwah nunua bei ghali akasema Simba na aliinunua miaka mitano ilopita, ukisema aondoke ataondoka na timu yake mzee. Mkuu unamfukuzaje owner ? . The Glazer family Owns man united kama majority shareholder huku Jim akiwa significant minority shareholder sasa Man u fans hawaitaki hiyo famili ya Glazer ila hawana la kufanya..
Mo hajainunua simba, ni ivi mo anamiliki 49% na simba 51%
Anawekezaje simba
Alisema kuwa atanunua bond bot za 20billion, hakafu faida itakayopatikana ndio ataendeshea timu
Je huo ni uwekezaji wenye tija?
 
Sidhani kama shida ni MO, Nadhani ni nmna usajili wa simba ulivyo na mgao wa madaraka kwa mujibu wa katiba na miongozo ya simba. Kuna ngazi nyingi za maamuzi yanayotoa mianya mingi kuidhibiti timu. Hata ungekuwa MO, kwa usajili wa Simba ulivyo autonomy ya timu ndogo kwa MO. Watu wanatumia mianya hiyo kula hela. Tofauyi sana na Yanga Muundo wake umenyoka.
Hamna wanaofanya maamuzi ni watu waliowekwa na yeye
Try again ni raisi wa club lakini yeye anatoka upande wa mo
Mangungu ambae ni kama bubu ndie anayetoka upande wetu wanachama
Sasa tutaachaje kumlaumu mo, wakati watu wake ndio wafanya maamuzi ya timu kitu ni kinyume na katiba yetu, na ndio maana mchakato umekwama
 
Back
Top Bottom