Haya ndiyo matokeo ya mikataba ya siri. Hakuna aliyekuwa anajua kwamba Simba ina mkataba na Mo. Kila mtu alikuwa anajua kwamba ni ile hali ya kuifadhili klabu. Kumbe kuna nkataba. Aveva aanze kutafuta pori la kujificha
Mdau mkubwa wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘MO’ ameiandikia klabu hiyo barua (demand note) ya kuitaka kumlipa fedha zote za mishahara alizokuwa akiwalipa wachezaji tangu mwaka jana kiasi cha shilingi bilioni 1.4 baada ya kubaini kuwa klabu hiyo imeingia mkataba na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.
Hayo yamejiri siku moja baada ya Simba kutiliana saini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa. Uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa timu, Evans Aveva, ulisaini mkataba huo wa miaka mitano na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.
MO amewaandikia Simba ‘demand note’ kwa kuwa wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe fedha kama makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.
Klabu hiyo ya Simba imeanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.
Kwani Mo ni mdhamini mmiliki au mwanachama wa kawaida tu? Mchakato wa umiliki wa klabu haujakamilika. Na hata ukikamilika huyo Mo atakuwa na 51% tu ya hisa sio kwamba atamiliki klabu moja kwa Moja.