Mnyukano CCM nini hatma yake?

Mnyukano CCM nini hatma yake?

Peter Stephano 809

Senior Member
Joined
Feb 29, 2020
Posts
120
Reaction score
162
Kuwepo kwa sintofahamu na mwendelezo wa kauli tatanishi baina ya Wanachama wa chama cha Mapinduzi, CCM ni Jambo jipya linalowavutia wengi kujua mwisho wake.

Baadhi ya watu hukitaja kitendo hiki kuwa ni mpasuko wa chama Cha Mapinduzi baada ya kifo cha hayati John Magufuli

na Wengine kufika mbali zaidi kuwa kuna uchu wa madaraka miongoni mwa wanaCCM Wengi.

Mapema tu baada ya kifo cha Magufuli baadhi ya Wanachama Cha Mapinduzi wakiwemo wabunge walianza kukosoa mwenendo wa utawala wa awamu ya 5 ambayo Magufuli aliiongoza kama Rais huku wengine wakimtetea na kusisitiza kuwa alifanya mengi mazuri aachwe apumzike kwa amani.

Kupishana kwa mitazamo ndiko kulionyesha kuwa ndani ya CCM Kuna makundi yaliyojijenga tofauti kiitikadi.

Haikuishia hapo tu baada ya Rais Samia kuchukua kiti cha Uenyekiti wa chama pamoja na Urais wa nchi amefanya mabadiliko makubwa kwenye Safu ya uongozi wa chama, Baraza la mawaziri jambo ambalo halikutarajiwa na wengi na ndilo lililo onyesha taswira mpya ndani ya CCM.

Na hapa ndipo filamu pendwa yenyewe ilipoanzia baada ya Wanachama walionekana kuwa na nguvu kushushwa na kuonekana si lolote, hakuna aliejua kesho ya Dkt Bashiru kutoka kwenye ukatibu mkuu CCM mpaka Ubunge wa Kuteuliwa, na hakuna aliyeijua kesho ya Hamphrey Polepole kutoka ukatibu uenezi CCM mpaka Ubunge wa kuteuliwa.

Huu wote ulikuwa mwanzo wa filamu pendwa inayo shuhudiwa hivi sasa ambayo ilimuweka kwenye ramani Hamdu Shaka kijana mdogo ambaye hakutabiriwa kuwa angekuja kuwa mkuu wa chama Cha akina Polepole yule wa "V Eite".
Filamu iliyotamu zaidi iliyomtoa jalalani Chongolo aliyekuwa anaambiwa kaa kimya na akina Makonda ni iliyo wapokonya ufalme wa Vijana akina Jerry Slaa.

Filamu hii pendwa iliyokolezwa na Shule ya Uongozi iliyoanzishwa na Hamphrey Polepole ndiyo inayotulewesha hivi sasa na kutufanya tuone siasa ni mchezo mchafu usio tabirika.

Shambulio dhidi ya Job Ndugai ni kama kionjo tu kwenye hii filamu pendwa yenye visa murua, hivi nani aliamini kuwa ipo siku Rais Samia asimame jukwaani kumsimanga Ndugai? Nani aliamini ipo siku Ndugai atakuwa miongoni mwa wanao kaangwa na sio wakaangaji?

Ndio utamu wa hii filamu unaporejea kila asiedhaniwa anaunga tela la uhondo.

Ni vigumu kutabiri upi mwisho wa filamu hii pendwa ya kisiasa ndani ya chama Cha Mapinduzi hasa ifikapo 2025.

Kina nani watawekwa kando wasubiri Vita ya 2025 Kama alivyosema Mama Samia, ni Jobu Ndugai, Polepole au kina Gwajima?.

Chukua kiti tuendelee kuitazama filamu hii pendwa ya Taifa.

Peter Mwaihola kitaaluma ni mwandishi wa habari na Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na jamii.
images%20(1).jpg
 
Jambo jipya?? Hivi ni lini CCM imewahi kuwepo bila mpasuko?! Waliokula chumvi za kutosha kidogo wanaelewa kuwa hiyo kwao ni mwendo wa kawaida tu…Hata kabla hakijawa CCM kulikuwepo ya akina Kambona na baadae, akina Bibi Titi, Aboud Jumbe, Maalim Seif, Kolimba, Mrema, Lowassa….n.k
Huo mtumbwi huwa unafika tu hata kama unaingiza maji..
 
Kuwepo kwa sintofahamu na mwendelezo wa kauli tatanishi baina ya Wanachama wa chama cha Mapinduzi, CCM ni Jambo jipya linalowavutia wengi kujua mwisho wake.

Baadhi ya watu hukitaja kitendo hiki kuwa ni mpasuko wa chama Cha Mapinduzi baada ya kifo cha hayati John Magufuli

na Wengine kufika mbali zaidi kuwa kuna uchu wa madaraka miongoni mwa wanaCCM Wengi.

Mapema tu baada ya kifo cha Magufuli baadhi ya Wanachama Cha Mapinduzi wakiwemo wabunge walianza kukosoa mwenendo wa utawala wa awamu ya 5 ambayo Magufuli aliiongoza kama Rais huku wengine wakimtetea na kusisitiza kuwa alifanya mengi mazuri aachwe apumzike kwa amani.

Kupishana kwa mitazamo ndiko kulionyesha kuwa ndani ya CCM Kuna makundi yaliyojijenga tofauti kiitikadi.

Haikuishia hapo tu baada ya Rais Samia kuchukua kiti cha Uenyekiti wa chama pamoja na Urais wa nchi amefanya mabadiliko makubwa kwenye Safu ya uongozi wa chama, Baraza la mawaziri jambo ambalo halikutarajiwa na wengi na ndilo lililo onyesha taswira mpya ndani ya CCM.

Na hapa ndipo filamu pendwa yenyewe ilipoanzia baada ya Wanachama walionekana kuwa na nguvu kushushwa na kuonekana si lolote, hakuna aliejua kesho ya Dkt Bashiru kutoka kwenye ukatibu mkuu CCM mpaka Ubunge wa Kuteuliwa, na hakuna aliyeijua kesho ya Hamphrey Polepole kutoka ukatibu uenezi CCM mpaka Ubunge wa kuteuliwa.

Huu wote ulikuwa mwanzo wa filamu pendwa inayo shuhudiwa hivi sasa ambayo ilimuweka kwenye ramani Hamdu Shaka kijana mdogo ambaye hakutabiriwa kuwa angekuja kuwa mkuu wa chama Cha akina Polepole yule wa "V Eite".
Filamu iliyotamu zaidi iliyomtoa jalalani Chongolo aliyekuwa anaambiwa kaa kimya na akina Makonda ni iliyo wapokonya ufalme wa Vijana akina Jerry Slaa.

Filamu hii pendwa iliyokolezwa na Shule ya Uongozi iliyoanzishwa na Hamphrey Polepole ndiyo inayotulewesha hivi sasa na kutufanya tuone siasa ni mchezo mchafu usio tabirika.

Shambulio dhidi ya Job Ndugai ni kama kionjo tu kwenye hii filamu pendwa yenye visa murua, hivi nani aliamini kuwa ipo siku Rais Samia asimame jukwaani kumsimanga Ndugai? Nani aliamini ipo siku Ndugai atakuwa miongoni mwa wanao kaangwa na sio wakaangaji?

Ndio utamu wa hii filamu unaporejea kila asiedhaniwa anaunga tela la uhondo.

Ni vigumu kutabiri upi mwisho wa filamu hii pendwa ya kisiasa ndani ya chama Cha Mapinduzi hasa ifikapo 2025.

Kina nani watawekwa kando wasubiri Vita ya 2025 Kama alivyosema Mama Samia, ni Jobu Ndugai, Polepole au kina Gwajima?.

Chukua kiti tuendelee kuitazama filamu hii pendwa ya Taifa.

Peter Mwaihola kitaaluma ni mwandishi wa habari na Mchambuzi wa Masuala ya Siasa na jamii.View attachment 2069577
CCM kina WENYEWE na hao ndio ambao sasa wanatawala nchi hii baada ya WAKUJA kutawala Awamu ya Tano. Vibaraka viongozi wanatumika tu
 
Back
Top Bottom