Mnyonge ni nani na vipi anatetewa?

Mnyonge ni nani na vipi anatetewa?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
17,572
Reaction score
27,314
Kumekuwa na hizi kauli za Mtetezi wa Wanyonge hivi karibuni..., Ila nadhani ni vema tukajiuliza myonge huyo ni nani na vipi anatetewa.

Binafsi nadhani myonge ni yule mwenye haki lakini hapewi haki yake na sio yule anayesaidiwa kuvunja haki / sheria sababu ya mapungufu / uhaba wa hiki au kile. Kwa hiyo kwangu mimi wanyonge ni wale ambao wamefanya kazi hawapewi au pension zao zinacheleweshwa, wana kesi hazisikilizwi kwa wakati, watoto wao wana akili/uwezo lakini hawapewi mikopo, ingawa wananchi wenzao wanalipa Kodi ila wakiugua wanakosa matibabu, ingawa serikali inakusanya kodi, hawapati huduma muhimu, wanatoa pesa/ wanakopeshwa ili wasome na wakimaliza wanaanza kudaiwa wakati walichosomeshwa hakiwafai/ hakiwezi kuwaingizia kipato (hao kwangu ndio wanyonge).

Wanyonge sio machinga wachuuzi (na kama ni wanyonge unyonge wao sio kuwa machinga) bali ni kwa nchi yao kukosa policies za kuwaondoa katika uchuuzi na kubangaiza / kubahatisha bila kuijua kesho yao, Pili kwa kuwaacha machinga waendelee kuchomwa jua kila kukicha bila kuwaandalia mazingira ya kuwatoa barabarani sio kuwatetea bali ni kwalaghai kwamba wao maisha yao pale ndio kikomo..., na kusema tu ninawapenda kwahio ninawaruhusu muingie popote (hata kama mnahatarisha maisha yenu) sio kuwapenda bali ni kutumia siasa/ propaganda na kuwahadaa.

Kama hio haitoshi watetezi hawa wa wanyonge wanaenda mbali zaidi ya kutengeneza chuki baina ya so called wanyonge na so called mafisadi/ wakwepa kodi (wafanyabiashara). Yaani badala ya hao watetezi wa wanyonge kuwashukuru wafanyabiashara wakubwa (so called wakwepa kodi) sababu wanatoa ajira kwa hawa wanyonge (kazi ambayo serikali imeshindwa) wanawaambia hawa wanyonge kwamba hawa ndio wakwepa kodi na wapiga deals, kwamba shida zenu sio sisi kukosa ubunifu bali ni wale walafi wanakula keki yote ya taifa.

Bila kujua ni vita gani tunapigana na nani tunapigana nae tunaweza kujikuta tunamalizana wenyewe kwa wenyewe wakati hao watetezi wetu ndio haswaaa hawafanyi kazi zao na hawatutetei bali wanatugombanisha.
 
Dah maada Kama hii ma great thinkers hawajaiona
 
Mnyonge ni matumbo ya Wanaccm na viongozi wao.
 
Naam wakati so called wanyonge (Machinga) ambao wengi wao sio machinga bali wafanyabiashara wasiofuata sheria na taratibu wanatetewa naomba tujiulize tena Myonge ni Nani ?

Kwa Kipindi hiki Myonge ni Mkulima aliyelima mahindi na Kukosa wateja..., Myonge ni mimi na wewe ambao tunabanwa na Matozo bila kupata Value for Money....
 
Okay myonge ni Mkulima.........

Je myonyaji ni mlaji anayelalamika kwamba bei haishikiki kulingana na kipato chake au ni serikali iliyosababisha gharama za uendeshaji kuongezeka na kutojitayarisha kwa uhaba uliopo ?
 
Naam wakati so called wanyonge (Machinga) ambao wengi wao sio machinga bali wafanyabiashara wasiofuata sheria na taratibu wanatetewa naomba tujiulize tena Myonge ni Nani ?

Kwa Kipindi hiki Myonge ni Mkulima aliyelima mahindi na Kukosa wateja..., Myonge ni mimi na wewe ambao tunabanwa na Matozo bila kupata Value for Money....
Hiyo Tafsiri ya Mnyonge kuwa ni Mmachinga umeitoa wapi ?
 
Back
Top Bottom