Jirani, samahani kwa kuchelewa kukupatia response kamili kuhusiana na haya mambo uliyoniuliza. Nimechelewa kufanya hivyo kwa sababu nilikuwa vijijini na pia nilikuwa natumia simu ambayo capacity yake ilikuwa ni ndogo.
Kwa kuanzia, for a long time nimekuwa nikifanya seminars, mikutano, workshops, et al ili kutoa elimu ya uraia kwa wananchi sambamba na kutoa elimu ya katiba hasa ikizingatiwa kuwa mimi binafsi nasomea sheria. Lengo kubwa ni kuleta awareness kwa wananchi ili waweze kuzitambua haki zao na pia wawe tayari kuzidai haki zao za msingi pale wanapoporwa na serikali/viongozi dhalimu.
Essentially ni kutoa elimu ya uraia kwa wananchi na pia kuendeleza operation ya M4C Iramba Mashariki. Kazi hii ni ngumu kutokana na ukweli kwamba kwa muda mrefu CCM imekuwa ikiwapumbaza wananchi ili wasitambue haki zao za msingi hivyo basi nimekuwa nikiji-engage ktk ku-change minds na attitudes za watu waliopumbazwa!.
Karibu kwanza ili tuendelee kujadili pamoja... pia uliza na maswali mengineyo