Fanyeni kama walivyofanya wale wa Ntwara... 'Gesi haitoki' iwe 'Maji hayapiti' nakuhakikishia mtapata hadi ya kumwagilizia nyasi..Sisi tunaoishi maeneo ya kimara hali sasa imeshakuwa mbaya sana. Ipo siku tutakapoona gari la Dawasco linapita tutachoma Moto. Hivi kama kweli kuna shida mahali ni kitu gani kinashindikana kutoa taarifa zinazoeleweka kwa wananchi. Kila mtu anajua maji ni kila kitu. Tumekuwa tukiuziwa maji ya chumvi ambayo nayo pia yanapatikana kwa shida na hata hatujui yanatoka wapi, sijui kwa mwarabu, huyu jamaa akiamua kutumaliza si tutakwisha wote. Kama kweli kuna tatizo mahali hasa linalochukua muda mrefu kwanini serikali isitafute njia mbadala ya kusaidia watu wanaoishi maeneo hayo!!. Ni kwamba huku hakuna viongozi wanaona hili. Haiwezekani watu hampati maji miezi miwili halafu mtu aseme eti wanatengeneza mitambo au njia za maji kwa muda wote huo. hii haiingii akilini.
Zimeni huo umeme wenu hatuutaki tupeni Maji.
Bomba la maji linapita kimara... sijui kwa nini hawa watu hawapigi hata MKWARA kidogo tu ili wapate maji?Wizara ya maji ipo hapo ubungo kwanini wakazi wa kimara msiende hapo mkawashinikiza hao wa watendaji wa wizara? Mh. Mnyika anajitahidi hata bungeni wakati wa bajeti ya wizara ya maji alimbana waziri lakni bajeti ilipita.
Dar yote ina matatizo ya maji, si maji safi tu hata maji taka..je huko kote chadema inahusika?Chadema haifai tuitoe tu, mbona tunajuta.
Fanyeni kama walivyofanya wale wa Ntwara... 'Gesi haitoki' iwe 'Maji hayapiti' nakuhakikishia mtapata hadi ya kumwagilizia nyasi..
Dar yote ina matatizo ya maji, si maji safi tu hata maji taka..je huko kote chadema inahusika?
Chadema haifai tuitoe tu, mbona tunajuta.
Mnyika angekuwa anapiga kelele za tatizo la maji kama afanyavyo kwenye shughuli za chama, wakazi wa jimbo lake wasingelalamika hivi, na mnyika akicheza tu 2015 watamuondoa kutokana na tatizo la maji.Dawa ni kuhakikisha mnyika hapati tena ubunge 2015 sababu toka aingie hamna alichokifanya zaidi ya kupiga blah blah
mbunge kazi yake nikuishauri serikali na kutunga sheria kazi yakuleta maji ni ya serikali so ilaumuni serikali ya ccm bwana na muihukumu 2014 na 2015
Hao wa mtwara walipata walichotaka?
Nimekwambia kama siyo tatizo la maji safi basi kutakuwa na tatizo la maji taka. Hilo ni tatizo dar nzima, si city center wala si Oysterbay. Chemba zinazovuja vinyesi ziko kila mahali... yule msanii aliyesema dar inanuka hakukosea.Wewe unadhani dar ndio ubungo? kuna sehemu hazina shida ya maji kama ilivyo ubungo.