VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kwanza nianze kumpa pole Mbunge wa Kibamba,John John Mnyika kwa kufiwa na baba yake mzazi. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Pamoja na kupatwa na msiba huo mkubwa,Mnyika alijumuika na Madiwani wa CHADEMA jijini Dar es Salaam kushiriki uchaguzi wa Meya. Uwepo wa Mnyika pale Karimjee ulikuwa na maana na uzito wake.
Mnyika aliwaambia makamanda wenzake kuwa,ingawa yuko kwenye majonzi ya msiba wa babaye,yuko pamoja nao katika kuandika historia ya kidemokrasia jijini Dar. Mnyika alikuwa Karimjee kumaliza kazi aliyoianza na wenzake. Kumaliza mapambano. Mwingine angepata kisingizio cha kutokuwepo Karimjee.
Naam,Kamanda Mnyika ni Commander of CHADEMA of the first degree. Anastahili pongezi. Hata ustawi na kutamba kwa CHADEMA hapa Dar hakuwezi kutenganishwa na Mnyika anayetaniwa kama kiboko ya UWT (Mama Hawa Ng'umbi na Dr. Fenella Mukangara).
Mnyika anastahili heshima kubwa kichama na kibunge. Kwa hoja za haja,yuko vizuri!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam