Mnyika na Wananchi wa Mbezi Mwisho waandamana kupinga X za kwenye Nyumba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,689
55,662
Wananchi Mbezi Mwisho na Mbunge John Mnyika wameandamana kupinga kubomolewa baada ya nyumba zao kuwekewa alama ya X.

Pamoja na Maandamano hayo, Mbunge John Mnyika ameweza kuongea na Wananchi wa Kibamba juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili kama wakazi wa Kibamba na Dar es Salaam kwa Ujumla wake.

MNYIKA AUNGURUMA JIMBONI KIBAMBA KATA YA MBEZI.
18555847_1349581465155627_1786607727060651292_n.jpg

18528025_1349583048488802_7846830223424006848_n.jpg
18425226_1349583375155436_5790779629735808712_n.jpg
18423859_1349582568488850_1875488788862118643_n.jpg
18447604_1349582061822234_4648379199334766010_n.jpg

Mhe John Mnyika leo alikuwa kwenye Ziara Kwenye Jimbo lake la Kibamba..

Mhe John Mnyika aliunguruma kwenye Viwanja vya Mbezi mwisho Stand ya zamani,

Wananchi wakiwa na Kiu ya kumsikia Mbunge wao, mhe John Mnyika alianza Kutoa nafasi ya Wananchi waulize maswali mbali mbali,

Na wananchi zaidi ya Tisa walijitokeza kuuliza maswali mbali mbali. juu ya ZOEZI LA BOMOA BOMOA linalofanywa na Serikali,

Mhe John Mnyika ameweka wazi kuwa juu ya Zoezi hilo yuko upande wa Wananchi,mana zoezi hilo haliwatendei Haki wananchi kwa kuvunja Nyumba zao bila fidia,

Juu ya Hoja ya Maji.Mhe Mnyika amewaambia wananchi kwa sasa Maji mabomba yamefungwa na kazi imekamilika.

Hivyo zoezi lililopo ni Maji yanapaswa yatirike kila eneo. Na kama kuna Eneo ambalo halitoki Maji ni Mtendaji mkuu wa Dawasco apewe Taarifa.

Kwenye Mkutano ambao uliudhuriwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob. Ambaye aliongelea hoja ya matibabu bure kwa wazee kwa Kutumia kadi ya ( TIKA.)

Yani tiba kwa kadi, eneo lolote ambapo Wazee wakiambiwa walipe pesa na watumishi wa zahanati/Hospital/Vituo vya afya watoe taarifa.

Kwenye Mkutano huo, Mhe Saed Kubenea Mbunge wa Ubungo naye alikuwepo kumpa Sapoti mbunge mwenzake John Mnyika.

Mhe Saed Kubenea aliongea kwa ufupi suala la Ushirikiano na Mbunge mwenzanke pale Bungeni kuibana Serikali, Katika Mkutano huo, Madiwani pamoja na Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa waliudhuria.

Kwenye Mkutano huo, alikuwepo Kamanda Mwnyeji wa Kata Mhe Humphrey Sambo, Mhe Sambo amewaambia wananchi kuwa bado atakomaa kuwatetea wananchi mpaka kieleweke,

MWISHO, Mhe Mnyika alimaliza kwa kutembea na Wananchi kwenda Kugagua maeneo mbali mbali yaliyoweka X.
 
wanajenga reli tena ya mwendo kasi,foleni haitakuwepo tena hapo mjini,ukizingatia kuna mwendo kasi pia.
 
Kila kzuri kina machungu yake
Mnyika usiwadanganye kuwa kuna namna nyingine ya kufanya,
Lazima Nyumba zibomolewe kama kweli maendeleo yanahitajika
Sasa swali hizo nyumba zikibomolewa leo, hiyo hela kujenga hiyo barabara ipo au kusubili miaka 7 ijayo?, kama hela ya ujenzi wa barabara kwa sasa haipo ni bora wasubili mpaka ipatikane, kuna watu huko kati ya makondeko na kibamba hospital walibomolewa nyumba zao kwa ajili ya kujenga satelite city, leo ni mwaka wa 8 hakuna kilichofanyika
 
Kuna zuri gani linafanywa na wapinzani?kila kitu kupinga hata kama kina manufaa kwao
Kutoka ubungo hadi chalinze km100,lakini inakuchukua masaa matatu kufika chalinze au Dar kisa ufinyu wa barabara,halafu mijitu inaandamana maana yake hawataki barabara?
Hizo barabara finyu zilijengwa n.a. upinzani?
 
Watu wa kulaumiwa zaidi ni Town Planners sijui wanafanya kazi gani??? Kila mara bomoa hii ingezuilika kama manispaa zingepima miji vizuri na pia hao ukawa kuna zingine wanaongoza waonyeshe mfano sasa..
 
Kwa foleni ya kudumu iliyoko maeneo hayo hakuna namna ni lazima barabara ipanuliwe. La muhimu wahusika walipwe fidia.
Thats a point bro...ila kama waliifuata barabara nao wafidiwe? Si yatakuwa yaleyale ya vyeti feki kuwa wapewe kiinua mfongo wakati ni wezi????
 
Back
Top Bottom