tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema kuwa madai ya kuunganisha mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ni tishio kwa uhuru wa uchaguzi nchini Tanzania.
Akizungumza Jumatano Agosti 27, 2025 katika mkutano wa mtandaoni ujulikanao kama Baraza la Kidigitali, Mnyika amesema muunganiko huo unaweza kuhatarisha usalama wa daftari la kudumu la wapigakura na kuacha mianya ya kuingiliwa na mamlaka za serikali.
Soma pia: Kwanini NIDA, INEC na CCM ghafla wamepanic na kuropoka ovyo ovyo kimfanano baada ya Pole pole kumwaga siri zao?
“Mjadala huu ulianza tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2020, na sisi kama CHADEMA tulionesha mashaka yetu kwamba kuunganisha mifumo hii miwili- NIDA na INEC kutafanya daftari la wapigakura kuwa chini ya mamlaka ya serikali badala ya tume huru,” amesema Mnyika.
Mnyika amerejea pia kauli ya kada wa CCM na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, ambaye hivi karibuni alidai kuwa mifumo ya NIDA, INEC na CCM imekuwa ikihusishwa ili kuhakikisha chama tawala kinashinda uchaguzi. Kauli hiyo ya Polepole ililazimu wakuu wa taasisi husika kujitokeza hadharani na kukanusha.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, alisema madai hayo “hayana ukweli wowote,” huku akisisitiza hakuna mfumo wa NIDA uliowahi kufungamanishwa na chama cha siasa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa INEC, Ramadhan Kailima, kupitia taarifa ya Agosti 23, 2025, alikanusha kuwa mifumo ya uchaguzi imeunganishwa na NIDA au chama chochote cha siasa.
Kailima aliongeza kuwa Tanzania haitumii mfumo wa kielektroniki katika kupiga kura wala kuhesabu matokeo, bali utaratibu wa kawaida (manual). Aidha, alisisitiza kuwa kitambulisho cha taifa hakitumiki kupigia kura, badala yake ni kadi ya mpiga kura pekee iliyotolewa na INEC.
Pamoja na utetezi huo, Mnyika amesisitiza kuwa hali hiyo inaonesha udhaifu wa mfumo wa uchaguzi wa Tanzania na akatoa wito kwa serikali kuandikisha upya daftari la wapigakura. “Wakati umefika sasa wa kusema imetosha. Tutake reforms na tuendelee na msimamo wa No Reforms, No Election,” amesisitiza.
Kwa mujibu wa CHADEMA, mageuzi ya katiba na uhuru wa tume ya uchaguzi ni miongoni mwa masharti ya msingi ya kupata uchaguzi wa haki na huru nchini.