Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 990
Acha wewe. wewe umetafiti nini? Amesema nini kuhusu Ubungo? Jimboni Mnyika ni mtupu mimi nalijua hilo kwa kuwa Mnyika ni Mbunge wangu. Mimi nimewahi kusema hapa Mnyika aitumie Ilani ya CCM kuwakandamiza sijui hataki kuisoma? Sijasikia akiwakumbusha watekeleze ahadi lukuki za barabara za jimboni Ubungo. Akisimamia hilo na barabara zile zikatengenezwa mbona atapeta tu mwaka 2015 lakini kinyume na hapo huenda akausikia Ubunge kwenye Bomba. Nyie mdanganyeni mkidhani mnamsaidia kumbe mnampoteza ati kinara; kinara wakati jimbo lake hali inatisha? wewe umewahi kupita barabara ya Kimara Mwisho kuelekea Kisukuru/segerea? Hali inatisha. Unaijua Bonyokwa wewe, Golani je, unaifahamu Kibangu ama King'ong'o au Kilungule. Utadhani hawakupiga kura hawa.
Najua hana pesa za kuleta maji wala barabara lakini hata kelele na kuwahamasisha watu wake. Mnyika ahamasishe tu barabara zile hazihitaji pesa nyingi na watu wa kule hawana makuu wewe pata grader la manispaa watajaza mafuta lichonge barabara. Awahakikishie watu kwamba atawaletea grader la manispaa waao wajitolee mafuta watu watatoa hela za mafuta na barabara zitachongwa; watu wa huko hawalalilii lami wao wanataka passability tu.
Mkuu watu wana ushabiki kama watoto vile bila kupambanua. Mimi nazijua siasa za Ubungo. Tunajua Mnyika alishinda kivipi na sababu za ushindi wake. Wacha tu wamdanganye kwamba mambo huko ni shwari, hatutakuwa na hata sababu ya kwenda kukesha Loyola kwa kuwa tutakuwa tayari tunajua matokeo.
Molemo nilijua utakuja tu tena nilitaka nikukaribishe. Mimi sina shida hata kidogo na JJ Mnyika. Namfahamu vizuri na sijawahi kumponda kwenye uchangiaji wake bungeni (kasoro ile ya dhaifu). Najua ni kijana makini na ana hoja makini za Kitaifa; sina shida na hilo. Tatizo langu ni kwamba Mnyika sasa arudi chini kwa watu waliomchagua aunganishe na hoja zake za kitaifa; asisahau waliompeleka huko kupata nafasi ya kuwa Kinara.Mkuu wewe siku zote hakuna jema analofanya Mnyika...Mimi ni mkazi wa Ubungo na huyu ndiye mbunge bora ukilinganisha na wabunge wengine kwa kipindi cha miaka 20
Mkuu M4C haitaacha mtu salama.CCM imeshikilia ubunge wa Ubungo miaka 50 huwalaumu bali unamlaumu Mnyika aliyeshika ubunge miaka 2
Molemo nilijua utakuja tu tena nilitaka nikukaribishe. Mimi sina shida hata kidogo na JJ Mnyika. Namfahamu vizuri na sijawahi kumponda kwenye uchangiaji wake bungeni (kasoro ile ya dhaifu). Najua ni kijana makini na ana hoja makini za Kitaifa; sina shida na hilo. Tatizo langu ni kwamba Mnyika sasa arudi chini kwa watu waliomchagua aunganishe na hoja zake za kitaifa; asisahau waliompeleka huko kupata nafasi ya kuwa Kinara.
Nipe Ubora wake jimboni. Afadhali hata Keenja kwenye awamu yake ya kwanza.
Kimsingi jimbo la Ubungo kupewa mnyika kulikuwa ni kumdhoofisha kisiasa anake jimbo enzi ya keenja lilikuwa na shida lukuki. maji ndo kabisa bara bara usiseme hakuna hata moja so kutegemea Mnyika afanye kwa miaka 5 ni uongo, keenja alikaa miaka mingapi? maji yalikuwepo?
Kimara iko kabisa na ubungo maji msewe yote na [size=+4]golani[/size] wanatumia maji ya mto maboamba hayatoi maji. bora hata ujio wa mnyika ulileta na miradi ya tasaf maeneo ya kibwegere na kwembe barabara ndo mbovu hazipitiki lol!
Kwembe hakuna njia, bonyokwa king'ong'o, kibwegere ndio afadhali kidogo na makabe
Ndiyo maana nasema acheni uvivu wa kusoma. Muulize Magufuli majibu ya Mnyika kuhusu kituo cha Ubungo na wakati mwingine anapavamia pale Ubungo bila watu kuwa na taarifa.
Ni nani aliyebuni kuwepo na barabara za pembezoni ili kupunguza foleni za Dar ambako jiji zima ni foleni kila kona.
Unaposema kuwa wewe ni mkazi wa Ubungo ukumbuke hii ni JF hujui anaye-press keyboard yuko wapi na si ajabu anaishi nyumba mnayotizamana. Na hilo si la msingi.
Na hivi vigezo ndiyo maana halisi ya mbunge. Mabunge hafukuzwi kwa sababu akirudi jimboni analala. Ubunge ni uwakilishi mle bungeni. Hiyo definition yenu ni wenye njaa wametuzoesha na ndiyo tunayopigania kuondokana nayo maana hakuna sehemu ya katiba ya nchi yoyote duniani inasema mbunge kazi yake ni tofauti na ile ya uwakilishi eti kwamba imegeuka kuwa mhimizaji au mchangia maendeleo.
Mbunge akikutana na wananchi ni kwa mujibu wa kujua kero ili akamkamate waziri husik kule bungeni. Tafiti zaidi usipende tukumegee.
Jaribu kurudisha akili nyuma ukumbuke maneno aliyomwambia Magufuli wakati anazindua kituo cha basi
Pia Mnyika kila anapomaliza mkutano wa bunge anafanya mikutano kila Kata kuchukua kero za wananchi kama wewe huhudhurii ni shauri yako hawezi kukufuata chumbani
Tatu naomba nikuambia watu wameichoka CCM na hilo ndilo la msingi zaidi.
Molemo mimi mbona namsifia sana Mnyika. Sina tatizo naye juu ya hoja zake. Najivunia kuwa na mbunge Kinara Bungeni tena siyo kwa kuangalia idadi ya michango tu bali contents za hiyo michango. Manake unaweza ukawa na michango mingi lakini pumba tupu; kwa Mnyika siyo hivyo.Mkuu laiti Mnyika angekuwa CCM ungemsifia vibaya sana....
Mkuu ni nani aliyebuni hizo barabara? Unamfahamu? Najua si Mnyika hata chembe. Yeye namshauri asimamie serikali kutekeleza ahadi ya chama tawala kuhusu hizo ring na bypass roads achilia mbali fly overs. Hapo najua utakuwa umetoka nje ya uwanja.
Kuhusu mbunge kusimamia serikali nalijua sana hilo ila katika hali ya sasa hilo peke yake halitamsaidia sana Mbunge. Mbunge anatakiwa ahamasishe maendeleo jimboni kwake ili wananchi chini ya uongozi wake wajiletee maendeleo. Mbunge ambaye ataitegemea serikali peke yake ilete maendeleo jimboni kwake hakika huyo si mbunge. Serikali ina vipaumbele ambavyo vingine ni tofauti na vya Mbunge na Jimbo. Wakati wabunge wanaomba kura na kutoa ahadi wakati wa kampeni walikuwa wamekubaliana na serikali kwamba nitatoa ahadi hizi kwa wanapiga kura wangu na serikali mtatekeleza kwa kuwa nitakuwa nawasimamia? Hapo ndipo hiyo gap inatakiwa izibwe na uhamasishaji ili wananchi wajiletee maendeleo.
Moja ya michango yake inayompa juckpot ni swali kuhusu ujenzi wa barabara ya Kilungile kwa hiyo usihofu. Pia fahamu serikali ya CCM ingependa kumrudisha nyuma katika maendeleo ya jimbo ili kumchonganisha na wananchi.Barabara Kilungule vipi?
Barabara Kilungule vipi?
big up Mnyika umejitahd sana. lakin je wafikiri ni kwanini hawa wabunge wa CDM wameweza kufikia hapo?