mr traders
Member
- Oct 27, 2012
- 38
- 15
BAADA ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuondoa hoja binafsi ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), kuhusu hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika jiji la Dar es Salaam, mbunge huyo amekata rufaa kupinga uamuzi huo.
Katika barua yake yenye Kumb: OMU/BJMT/013/2013 iliyowasilishwa kwa Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam, Mnyika ameomba rufaa dhidi ya uendeshaji wa Bunge usiokuwa wa haki wa Naibu Spika Ndugai.
Mnyika alisema kuwa Ndugai alikiuka kanuni ya 58 (5) kwa kulihoji Bunge kinyume na kanuni na kufanya uamuzi batili wa kuondoa hoja yake hiyo.
"Tafadhali rejea kumbukumbu rasmi ya Bunge (Hansard) za kikao cha tano cha Februari 4, mwaka huu, cha mkutano wa kumi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Katika mkutano huo Naibu Spika Ndugai alisema na kufanya maamuzi: ;Sasa ninahoji wanaoafiki kwamba hoja hii iondolewe waseme ndiyo…..hoja imeondolewa. Walioafiki Wameshinda!'
"Wakati mtoa hoja sikuwa nimeomba idhini yoyote ya hoja yangu kuondolewa."
Mnyika aliongeza kuwa maamuzi hayo ni kinyume na kanuni ya 58 fasili 5 ambayo inaelekeza: "Endapo hoja imefikishwa bungeni, mtoa hoja anaweza tu kuiondoa hoja yake kwa kusimama mahali pake na kusema, ;Ninaomba ruhusa kuondoa hoja'.
Papo hapo, Spika ataliuliza Bunge kama linaafiki hoja hiyo kuondolewa na inapotokea wabunge walio wengi watakubali, Spika atasema hoja hiyo inaondolewa kwa idhini ya Bunge' na hoja hiyo itakuwa imeondolewa na Bunge litaendelea na shughuli inayofuata.
Katika rufaa yake hiyo, Mnyika aliambatanisha ushahidi wa kumbukumbu rasmi za Bunge (Hansard) za kikao tajwa ili kuthibitisha ukiukwaji huo wa kanuni.
Alisema kuwa pamoja na kuwa kanuni ya 8 inataka Spika kuendesha shughuli za Bunge na kutoa maamuzi kwa haki, uadilifu na bila chuki wala upendeleo wowote kwa kuongozwa na Katiba ya nchi na kanuni za Bunge, Ndugai alifanya maamuzi yenye kukiuka kanuni ya 58 fasili ya 5 kwa kuruhusu hoja yake kuondolewa kwa hoja iliyowasilishwa na Waziri wa Maji.
"Naomba Spika ataarifiwe kwa mujibu wa kanuni ya 5 (4) na kuitisha kikao cha kamati ya kanuni kwa mujibu wa kanuni ya 5 (5) ya kanuni za kudumu za Bunge na kulijulisha Bunge kuhusu uamuzi utakaotolewa," alisema Mnyika.
Tanzaia Daima