katika kile kutimiza wajibu
wake wa kuisimamia na kuishauri serikali kamanda wa ubungo John Mnyika
ameendelea kutekeleza ahadi. jana katika pitapita yangu nimekutana barua
kutoka ofisi ya mkurugenzi yenye kuwajulisha kupokea fedha za mfuko wa
kuchochea maendeleo ya jimbo (cdcf), kwa jimbo la ubungo.
Fedha hizo hutolewa baada ya kamati ya kusimamia mfuko ambayo mwenyekiti
wake ni mbunge, walipokea maombi ya mradi kutoka kata na kamati
ikapitia maombi na baada hapo wakapitisha baadhi ya miradi na hii ni
kutokana na kiwango cha fedha kinachopokea kutoka serikali kuu. ambayo
kwa jimbo la ubungo inapokea kiasi cha sh.70milioni kwa mwaka.
Na hii ni miradi imepelekewa fedha ktk kata na kuanza utekekelezaji mara
moja.
1. Fedha Tsh. 10,500,000.00 kwa ajili ya kukarabati visima 3 vya maji
(mbadeco, kwa bi Asia na Anna Mkapa) na ujenzi wa kalvati eneo la
National Housingi- Mburahati.
2.Fedha Tsh.10,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha waenda kwa
miguu eneo la ubungo islamic sec school mtaa wa kibangu kata ya
makuburi.
3. Fedha Tsh. 10,000,000.00 kwa ajili ya umaliziaji wa choo cha shule ya
sekondari ya gogoni-kibamba
4. Fedha Tsh. 12,000,000.00 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 120 kwa
ajili ya shule ya msingi ukombozi,manzese,uzuri na kilimani-kata
manzese.
5. Fedha Tsh. 6,000,000.00 kwa ajili ya kuchangia mradi wa ujenzi wa
daraja linalojengwa kwa nguvu ya wananchi katika mtaa wa kanuni, kata ya
mabibo.
6. Fedha Tsh. 7,500,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vivuko vitatu
vinavyounganisha mitaa 5 kwa jongo. sisi kwa sisi, kilimahewa, kagera na
mianzini kata ya makurumla.
7. Fedha Tsh. 10,319,663.00 kwa ajili ya umaliziaji wa kituo cha polisi
msewe na ujenzi wa kalvati la waenda kwa miguu eneo la kibo, kata ya
ubungo.
8. Fedha Tsh. 3,500,000.00 kwa ajili ya kuchangia mradi wa maji kata ya
msigani.
9. Fedha Tsh. 12,000,000.00 kwa ajili ya ununuzi wa madawati 120 kwa
shule ya msingi msumi, kata ya mbezi.
N.b kwa kata ambazo hazikupata fedha zitazingatiwa kwa fedha za mfuko wa
jimbo kwa mwaka huu wa fedha.
Nawasilisha.