Mnyang'anyi na matendo halali

DMmasi

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
609
Reaction score
965
Salam

Tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga, naam uko msemo wa mtaani unasema "mwizi akiibiwa anaumia zaidi ya mtafutaji halali" labda ni sahihi sababu njia anayotumia kujitafutia ameshaibariki kama tendo halali la kujipatia umiliki.

Wanyang'anyi, ndio hawa kwa matendo yao na ukwapuzi wao hujipa umiliki halali na wanapookotewa mawe huwaita wale wanaotaka kuwaponda vichwa wakorofi, wahaini, wajinga, na mengine kwa kadiri ya maagizo yatokayo kwenye bongo zao kupitia ndimi zao.

Fisi halindi bucha mjomba, walisema wazee ila hawakusema alinde nani, na haiwezekani awe mbuzi wakati nduguye ndie aliyening'inizwa na wasemi wameshasema "uyu akinyolewa yule zake azitie maji" auuuuuh! analinda fisi aliyeshibishwa kwanza auuuuh! aliyetolewa meno.

Wanyang'anyi wameipenda dhambi hivyo wamechukia kitubio, mbaya zaidi ukiipenda dhambi yao na ukitaka kiti kwenye meza yao wanakupa vyeo kama afisa ukorofi, Dr uhaini n.k

Adios Amigo
 
Ukizoea Haram unajisahau kama ni Haram, baadae kuja kushtuka it's too late. Ndio unaanza kuhalalisha Haram.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…