Nyaka-One
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 4,628
- 6,563
Wadau, mwenzenu miaka kadhaa iliyopita nilinunua shamba sehemu fulani. Wakati wa kununua hilo eneo alikuwepo muuzaji, dalali wangu, mjumbe wa mtaa (maarufu kama balozi), watu wa serikali ya mtaa (mwenyekiti, katibu, mjumbe, afisa mtendaji wa mtaa), familia ya muuzaji, majirani mpakani mwa eneo, mashahidi wangu na onlookers wengine.
Kwa ajili ya kumbukumbu nilihakikisha narekodi picha za video, picha za mnato na wakati mwingine sauti pekee yake wakati wa kuonyeshana mipaka, kulipana na kusaini mikataba.
Sasa tatizo lililopo ni kwamba miezi kadhaa iliyopita kuna mtu kaibuka na kumega sehemu ya hilo shamba na kuanza kujenga msingi. Baada ya kuwasiliana nae amedai aliuziwa na jamaa yule yule aliyeniuzia. Baadae nikaambiwa na msamaria mwema kwamba ni kweli huyo jamaa aliuziwa kwa kuwahusisha watu wa serikali ya mtaa na kwamba walichofanya ni kuandika tarehe ya nyuma kwenye mkataba ili ionekane kwamba yeye ndiye alinitangulia kununua eneo hilo.
Kwa vile nategemea kufuata utaratibu wa kisheria ili kupata haki yangu naomba msaada wenu wadau kama kuna sehemu ambayo naweza kupata huduma ya haraka ya "ink dating" ambako wino ulio kwenye karatasi za mkataba wa yule mnunuzi wa pili unaweza kufanyiwa analysis na hivyo kujua tarehe halisi mkataba wake uliposainiwa badala ya hizo tarehe walizofoji kwenye mkataba wake. Pia ushauri mwingine wowote kuhusu sakata hili unakaribishwa kwani naamini unaweza kuwa wenye manufaa kwa wengi.