MNEC Ndele Mwaselela: Viongozi tushuke kwa Wananchi kusikiliza Kero zao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,076
1,001
Na Mwandishi Wetu

Mkurugenzi na mmiliki wa Shule za Sekondari za Patrick Mission na Paradas Mission ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (M-NEC) Ndugu Ndele Mwaselela, amejipambanua kuwa kiongozi atakaye endelea kuyafikia makundi mbalimbali ya watu wenye vipato vya chini.

“ Furaha yangu ni kuhakikisha nagusa makundi mbalimbali na kuwa kiongozi ambaye nashuka chini kwenye jami, maana huko ndiko kwenye watu wengi na changamoto lukuki ambazo zinahitaji utashi na upendo wa hali ya juu kwa sisi viongozi tuliopewa dhamani kuzisikiliza, kuzichukua na kuzitatua pale inapobidi” Mwaselela

Amesema hayo tarehe 25 Mei 2024 wakati akizungumza na vijana zaidi ya 400 kutoka makundi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya ya Mbeya wakati wa chakula cha jioni kilicho andaliwa na kiongozi huyo.

Mwaselela amesema kuwa ameamua kumuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu hasani, ambaye anasisitiza viongozi kuonyesha upendo kwa wananchi kwenda kusikiliza na kutatua changamoto zinazo wakabili.

Tangu Rais Samia ameingia madarakani Machi 19,2021 amekuwa na falsafa yake ya ” R” nne (4R) anazozitumia katika utawala wake, 4R maana yake ni maridhiano (Reconciliation), mabadiliko (Reforms), ustahimilivu (Resilience), na kujengwa upya (Rebuilding).

“Kwahiyo pasipo kujali, tofauti ya vyama vyetu vya siasa, rangi wala kabila mimi nimejipambanua kuwa kiongozi ambaye rafiki zangu wakubwa ni wananchi wa kawaida ambao nitahakikisha nasikiliza kero zao na zingine ambazo nitazimuda nitazifanyia kazi ili nitimize kusudio langu la kumsaidia Mheshimiwa Rais Dokta Samia kwa vitendo” Mwaselela.

Kwaupande wao baadhi ya vijana ambao wamejitokeza katika hafla hiyo ya chakula cha jioni ukumbi wa Tughimbe ulipo mji mdogo wa Mbalizi, wamemshukuru Ndele Mwaselela kwa moyo huo wa pekee, wa kukubali kushuka kwa watu wa chini na kuonyesha upendo wake.

Kupitia tukio hilo vijana pia wamepata nafasi ya kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazowakabili sehemu za kazi zao, huku wakitoa shukurani kwa serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi kadhaa ya maendeleo ndani ya mkoa wa Mbeya na taifa kwa ujumla.

Aidha Mwaselela ameahindi kutoa mikopo kwa mama ntilie 100, kudhamini mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wa Mbeya Vijijini, kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni thelathini (30,000,000).

WhatsApp Image 2024-05-27 at 02.24.11.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-27 at 02.24.12.jpeg
 
Back
Top Bottom