GE2025 Mndeme: Tunahitaji Kigamboni isiyokuwa na vikwazo

GE2025 Mndeme: Tunahitaji Kigamboni isiyokuwa na vikwazo

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni, Jijini Dar es Salaam kupitia tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Wakili Mwanaisha Mndeme ameahidi kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa Mbunge wa jimbo hilo, atakuwa sauti ya wananchi katika kuibua, kufuatilia na kutatua changamoto zinazowakabili kwa muda mrefu.

Soma pia: Wakili Mwanaisha Mndeme atangaza kugombea Ubunge jimbo la Kigamboni kupitia ACT Wazalendo. Ataweza kumrithi Ndugulile?



Akizungumza na wananchi wa Kata ya Bada katika mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya jana Septemba 12, 2025, Mndeme alieleza dhamira yake ya dhati ya kuleta uwajibikaji, ushirikiano na maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Kigamboni.

Akiwa katika kampeni hiyo, alieleza kuwa bado sehemu kubwa ya wananchi wa Kigamboni wanaishi maisha ya kusuasua, hali inayohitaji mabadiliko ya haraka na yenye tija.

Wakili Mndeme ameendelea kufanya mikutano mbalimbali ya kampeni kunadi Sera zake pamoja na kusikiliza maoni ya wananchi, huku akisisitiza kuwa ajenda yake kuu ni kuhakikisha Kigamboni inakuwa sehemu salama, yenye maendeleo jumuishi na fursa sawa kwa wote.
 
Back
Top Bottom