Mnaowadharau watumishi wa Umma, Mungu anawaona

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,331
14,259
Wakuu heshima zenu!

Mimi ninayeandika Haya naomba kudeclare interest kwamba pia ni Mtumishi wa Serikali yetu. Kinachonisikitisha, ni namna Watu mbalimbali wanavyotoa Kauli za Kuwadharau, Kuwabeza na Kuwapuuza Watumishi. Fikiri Matharani Mtu anasema kwamba Watumishi kwanini wadai nyongeza ya Mishahara wakati hakuna wanachozalisha. Kauli hii peke yake inaweza kushusha Morali ya kufanya Kazi, Binafsi Sina Shida na Serikali maana najua Yapo Majukumu mazito yanayolikabiri Taifa, mbali ya Nyongeza za Mishahara, najua Serikali inatupenda sema tu Mambo ni mengi.

Lakini swali kwanini Watu mnatudharau? Kosa letu ni lipi? Sasa Mlitaka tufanyeje ili mridhike kuwa sisi ni wa maana kwenu? Ndugu Zangu Si kila Kazi inayofanywa na Mtumishi wa Serikali lazima ionyeshe Matunda hapo hapo, Zipo kazi huonyesha Matunda baada ya muda mrefu mfano, Kazi ya Walimu, Maafisa Ugani, Ustawi wa Jamii, Utafiti, n. K. Huleta Matunda baada ya Muda Fulani kuwa umepita,ni Tofauti na Sekta km vile Viwanda, Afya, Kodi, n. K. Ambazo huleta Matunda on the spot.

Jamani hivi kuna watu humu wanawadharau hata Walimu, Mimi Naona mnatenda Dhambi, kwasababu hata Hiyo Jeuri na Kiburi cha Kuandika hapa ukimdharau ni kutokana na Kazi ya Mwalimu huyo unayemdharau na kumbeza kwa si lolote. Wewe unayemdharau Daktari, unafanya hivyo kwasababu uko vizuri Kiafya, subiri Ukamatwe na homa Kali tuone km utaweza kushika hata simu au Kompyuta, thubutu yako badala yake utabaki ukimlilia daktari akusaidie, Lkn sasa wajitia kiburi kuwa Hawa si chochote, haya bhana ipo Siku, MUNGU anakuona tu na huo mdomo wako.Wengine wamewadharau kada ya Kilimo kwamba hata layman wa kijijini aweza kuwa mtaalamu wa Kilimo, OK!

Sawa, lakini mbona yakizuka Magonjwa yale hatarishi kwa Mazao mnawakimbilia na kuwaomba Ushauri namna ya kuyatokomeza? .Mbona Ukame ulipo ikumba nchi msimu uliopita mlikuwa mkisisitiza kuwa Watafiti wa Kilimo wajitahidi kuzalisha mbegu za muda mfupi na zinazovumilia Ukame na Magonjwa?, Kwanini basi msingewaambia Hao layman wa Vijijini wawazalishie mbegu hizo?

Jamani acheni Dharau kwa Watumishi. Kutokana na Kauli za Wengi zinafanya nikumbuke ule msemo wa "NJAA MWANA MALEGEZA, SHIBE MWANA MALEVYA".Watu wakiwa ktk Hali ya Raha isiyo na mikiki mikiki yoyote ile wanaweza KULEWA na kumdharau kila mtu, ndio maana Baadhi ya watu waliojikinai na kulewa Maisha mazuri hudiriki Kusema "HAKUNA MUNGU ".Hiyo yote ni kwasababu hawana shida na wakitaka chochote wanakipata. Hawa hawatofautiani Sana na Wanawadharau Watumishi kwasababu Wao Wamejitosheleza na km sio kujitosheleza basi tuseme hawajawahi kutana na Shida kubwa iliyohitaji Msaada wa Mtaalamu Fulani wa Sekta fulani Serikalini.

Wacha nisiwachoshe. Ombi langu kwenu ni Moja, naomba TUHESHIMIANE, Kila Mmoja anao umuhimu, Km ambavyo MUNGU alituumba na kutuweka Dunia kila Mmoja kwasababu fulani na MUNGU alijua kuwa kila mmoja ana umuhimu wake Vivyo hivyo hata ktk Maisha, Kila mtu anao umuhimu wake, Mtumishi wa Kada yoyote ile ana umuhimu wake ndio maana Kada hiyo iliwekwa ili watu waisomee na waitumikie, halikadhalika Mwananchi wa kawaida naye anao umuhimu wake, Mmoja akikosekana, lazima Mkwamo wa mambo Fulani utokee tu.

Asanteni.
 
Hapana, CCM mnaionea kabisa, Tuna miaka mingi tunafanya nayo Kazi wala hawajawahi kutamka Hadharani kwamba Watumishi hawazalishi chochote hivyo wasiongezewe Mishahara, Bali wao husema Bajeti haitoshi kutuongezea Mishahara nasi huwa tunawaelewa vizuri tu, maana cha muhimu ni Heshima na si swala la Malipo au lah!. Maana Heshima ni Kitu Bora Kuliko hata Fedha. Watu wa humu ndio wanaotudharau .
 
Hapana, CCM mnaionea kabisa, Tuna miaka mingi tunafanya nayo Kazi wala hawajawahi kutamka Hadharani kwamba Watumishi hawazalishi chochote hivyo wasiongezewe Mishahara, Bali wao husema Bajeti haitoshi kutuongezea Mishahara nasi huwa tunawaelewa vizuri tu, maana cha muhimu ni Heshima na si swala la Malipo au lah!. Maana Heshima ni Kitu Bora Kuliko hata Fedha. Watu wa humu ndio wanaotudharau .
Hivi huelewi?? Kinachofanyika hapa ni kwamba upinzani umeamua kutukana wafanya kazi wa serikali kwa hasira tuu.
Wanasahau kuwa kuna wafanya kazi wa serikalini wanaoupambania upinzani kufa na kupona.
Imani ya waliowengi ni kwamba kila mfanya kazi wa serikali ni mwanachama wa ccm

Hakuna aliyekikosa kitu
Halafu akakisifia mkuu
 
Tatizo hao wanaodharau hawajua tumetoka wapi hvo hawaelewi mchango wa watumishi wa umma nchi hii. Mfano mdogo ni kwenye IT ambapo sasa huduma nyingi za serikali unaweza kuzipata online pamoja na malipo mbalimbali tofauti na zamani ilibidi upange foleni ndefu. Kuna maeneo mengine mengi tu.
 
Watumishi kama wewe ndio mnafanya watumishi wadharaulike.

Mimi nimeishia kusoma hapo ulipo andika serikali ina majukumu mengi kwahiyo ni haki watumishi wasiongezewe mshahara...

Serikali ina majukumu ya kitaifa, kwani watumishi wa umma hawana majukumu ya kifamilia, kumbuka gharama za maisha zinapanda kila leo
 
Watumishi kama wewe ndio mnafanya watumishi wadharaulike.

Mimi nimeishia kusoma hapo ulipo andika serikali ina majukumu mengi kwahiyo ni haki watumishi wasiongezewe mshahara...

Serikali ina majukumu ya kitaifa, kwani watumishi wa umma hawana majukumu ya kifamilia, kumbuka gharama za maisha zinapanda kila leo
Huo ni mtizamo Wangu, Naamini hivyo, nawe unaamini jinsi unavyoamini.
 
Watumishi ni zaidi ya mafisadi wa ccm yani wao wanawaza kula sadaka tu na kunenepesha mke,watoto,mahawara zao...yani hawana imani kabisa istoshe yeye kila kitu mali yke kuanzia kanisa mpka sadaka.dini haina hosp au shule wala haijawahi kusaidia jamii hilo kanisa la majambazi anaetumia mdomo kuibia watu
Pole sana naona una hasira na watumishi wa Mungu hadi unajikurupukia tu kukomment. Uzi umesoma lakini braza?
 
Back
Top Bottom