Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 553
- 797
Nimeandika hili kuwatahadharisha ndugu zangu msirudie makosa baada ya mimi kupata majanga.
Nakumbuka mapema mwaka jana walikuwa na Promotion ya Xsmas pale Uchumi Supermarket Nyerere road,nilidakwa na wadada waliowavalisha uchi mlangoni wakanidanganya sana kwamba nikinunua simu kwao nitapata muda wa maongezi wa kuongea bure mwezi mzima na warranty ya miaka 2.
Baada ya kuzungukwa na kushawishiwa sana kwavile nilienda kununua simu na sikuamini kuwa kampuni kubwa kama hii inaweza kujiingiza kwenye mambo ya kitapeli nilikubali nikaenda kununua Samsung Galaxy J7 kwenye banda lao la promotion baada ya kuongea na msimamizi wao kwa kirefu na kuniaminisha vitu kumbe kampuni imeshageuka genge la matapeli.
Tatizo lilianza nilipowaomba waniunganishe kabisa nipate huo muda wa maongezi na meseji ya utambuzi wa Simu kutoka Samsung wakaniambia nilipie kwanza,nikalipia wakachana box la simu mpya wakaanza configuration zao baada ya kama dk 20 wakanipiga Sound kwamba Network iko down ila niende hadi usiku ntakuwa nimeshapata meseji nisipoiona kesho yake nirudi.
Kwavile walikuwa wameshachana mabox ya simu na walikuwa wakiongea kwa ushawishi sana na niko kwenye duka lao hadi Boss wao anasapoti nikawaamini nikachukua simu nikaondoka nikitegemea baadae ntapata hizo meseji,bahati mbaya hadi asbh sikupata meseji,nikarudi pale yule Boss wao akaniambia kuna matatizo makao makuu watu wameiba sana muda huo wa maongezi hivyo wameingiza password ni watu watatu tu wana hizo password hivyo wamezidiwa niwe na subira.
Niliondoka nikafuatiliafuatilia karibu wiki moja sound zilikuwa ni hizohizo na maneno ya ujanjaujanja mwingi na huyo mtu wao walionitambulisha kuwa ni wa Samsung,baadae nilichoka na kwa vile nilikuwa naitumia simu nilishindwa kuwarudishia nikaamua kufanya mambo yangu simu ilikuwa haina tatizo lolote.
Baada ya mwezi mmoja simu ikaleta matatizo nikajua ina warranty nikaipeleka Samsung,wakaicheki wakaniambia simu ni ya kwao kweli wakaiangalia tatizo wakaniambia LCD ndiyo imekufa na kwa vile simu hizo ni mpya itakuwa ndani ya Warranty,akasema wameishiwa LCD hivyo wanaiagiza Korea baada ya mwezi mmoja na nusu itafika watanipigia.
Baada ya Mwezi mmoja na nusu walinipigia kweli nikawapelekea simu,wakaanza matengenezo ila baada ya kuiangalia warranty yake vizuri wakagundua ni ya Muscat siyo Africa,wakawasiliana na Maboss wao wakawaambia simu irudishwe Zain ipelekwe huko Muscat la sivyo nilipie hiyo 350 ya LCD wao wanaservice simu zenye warranty ya Africa.
Kwahiyo nimekwama nimetapeliwa huo muda wa maongezi wa mwezi mzima na nimepewa warranty ya kiujanjaujanja ambayo pia naona kama ni utapeli pia,mwenye ushauri unaoweza kunisaidia pls.