Mnaoishi Arusha msaada jamani

Miss Jay

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
211
174
Habari wana jamvi,,,,,nina ndugu yangu amehamishiwa kikazi jijini Arusha na hajawahi kabisa kufika huko.Kwa mujibu wa maelekezo ya bosi ameambiwa aripoti kazin kabla ya tarehe 1 february sasa naombeni mnisaidie kujua baadhi ya mambo ambayo yatamsaidia kwenda kuanza maisha huko ugenini

1.yupo single na hana familia kwaiyo anahitaji chumba kimoja tu cha kupanga ila kiwe kizuri na kiwe ni self sasa naomba mnisaidie makadirio ya bei ya chumba cha aina hiyo ni sh ngapi kwa mwezi au kwa mwaka na utaratibu wa kulipa ukoje kama ni kwa mwezi au miezi 6 au ni mwaka

2.hawezi kusafiri na vyombo maana ni gharama kwaiyo napenda kujua bei ya kitanda kizuri cha 5*6 kwa Arusha kinaegemea bei gani,,,nikipata bei ya kitanda cha chuma na mbao vyote itakua vizuri,,,pia godoro zuri la 5*6 nchi 6 au 8 linaegemea bei gani

3.Mitaa mizuri ya kuishi kwa arusha ni ipi namaanisha isiwe uswazi wala isiwe uzunguni sana wanakoishi matajiri

4.Mhusika ana salon ya kike anataka ahame nayo kwaiyo napenda kujua chumba kizuri kikubwa cha biashara kinachofaa salon inaweza kuwa ni bei gani kwa mwezi?

Asanteni sana wanajukwaa na samahani kwa kuwauliza maswali mengi,,,lakin natumai majibu yenu yatakuwa msaada kwa maisha mapya ya ndugu yetu,,,Heri ya mwaka mpya 2017
 
Mkuu

1)Arusha vyumba si being ghali kama dar, 80k anapata chumba kizuri tu maeneo mengi mazuri

2) kitanda na godoro aandae 400k

3)hii inategemea atapata eneo gani la biashara, nadhani itakua busara ikiwa si mbali na eneo la kazi

4)bei zinatofautiana kulingana na eneo,kama ni mjini asisahau kuja na 'kilemba'

Sikai huko ila ni nyumbani so najua machache

Heri ya mwaka mpya
 
Kilemba ni nini mkuu???hapo sijakuelewa.Lakin pia asante kwa maelezo ulionipa
 
Kilemba ni nini mkuu???hapo sijakuelewa.Lakin pia asante kwa maelezo ulionipa
Mkuu kama ni frame za katikati ya mji wana haka kamchezo, yani unamlipa kiasi fulan aliyetoka, na wewe ukija kutoka utalipwa na anayeingia,

Nliwahi tafuta frame mjini nikakutana na huu upuuzi, eway karibu utajionea mwenyewe

Arusha pazuri,ukiwa vizuri na biashara utarudi tajiri mkuu
 
Back
Top Bottom