Mnaishije na mabosi wenu jamani???

vumilia ndg usiache kazi kabla haujapata kwingine ila lalamiko lako la kutaka kwenda lunch pamoja halijatulia
 
Pole sana ndugu,
nakushauri uongeze bidii katika kazi zako. Ukikutana na bosi wako mpe tabasamu la usoni hata kama moyoni huridhiki.
Hutakiwi kumkwepa wala kumuogopa, inabidi uwe nae karibu (kikazi) ili ujue nini anapenda nini hapendi.
Umesema amepandishwa cheo hivi karibuni? Inawezekana ana kiulimbukeni cha ubosi au hofu ya kufukuzwa kazi kama mambo hayotoenda vema.
Hivi wadau, maofisi hatutakiwi kuvunja ukimya? Kama vipi zungumzeni nae khs hilo.
 
pole sana mkuu....
lakini hayo ndo maisha si kila mtu anakupenda...
ila nakuonea huruma sababu ni bosi wako.....
we mwonyeshe ukarimu tu, hata mwalike nyumbani kwako kwa dinner....
vitu vidogo kama hivi vya weza saidia.....
kingene kama we unaelewana na wafanya kazi wengine hapo...itakuwa vizuri na itakusaidia kuskuma siku zako .....

PLAY SAFE.........
 
Show him love, obedience and respect - it will drive HIM CRAZY. Unaweza kushangaa yeye ndo anaweza kukimbia ofisi na kuwaacha nyie mnadunda.

1. Tunza mawasiliano yenu kwa maandishi. Kama mnadiscuss nae kitu, mkimaliza, mtwange email....folloiwng today's discussion etc..

2. Kama anakupa assignment kwa email hakikisha ukimjibu unacopy na wengine ili asijesema hutimizi wajibu wako au kazi yako ilikuwa mbovu

3. Kama anakupatia kazi flani na wakati huo huo unafanya kazi nyingine, mwambie politely kazi unayofanya wakati huo na kama anaridhia uipige chini ili ufanye anayotaka yeye. Kama watu wengine wanasikia, ni poa. Kama hakuna mtu, mtumie email ili kuweka kumbukumbu asije kukugeuka siku za usoni!

4. Be smart, work on agreed targets and meet your deadlines

5. Usipanic na wala usimuonyeshe kwamba anakutesa.
 
Ghafla katubadilikia, ni mateso bila chuki na mie sio mvumilivu wa manyanyaso,

Pole sana mkuu kwa yanayo kupata lakini binafsi sijaelewa aina na mateso unayo pata au mnayopata maana inaonyesha kama kitu mfanyiwacho ofisi nzima.Pili nakushauri kufuata taratibu za kazi kama mlivyo kubaliana kwenye mkataba wa ajira vinginevyo ungana na wenzio kudai haki zenu.
nawakilisha.
 
Show him love, obedience and respect - it will drive HIM CRAZY. Unaweza kushangaa yeye ndo anaweza kukimbia ofisi na kuwaacha nyie mnadunda.

1. Tunza mawasiliano yenu kwa maandishi. Kama mnadiscuss nae kitu, mkimaliza, mtwange email....folloiwng today's discussion etc..

2. Kama anakupa assignment kwa email hakikisha ukimjibu unacopy na wengine ili asijesema hutimizi wajibu wako au kazi yako ilikuwa mbovu

3. Kama anakupatia kazi flani na wakati huo huo unafanya kazi nyingine, mwambie politely kazi unayofanya wakati huo na kama anaridhia uipige chini ili ufanye anayotaka yeye. Kama watu wengine wanasikia, ni poa. Kama hakuna mtu, mtumie email ili kuweka kumbukumbu asije kukugeuka siku za usoni!

4. Be smart, work on agreed targets and meet your deadlines

5. Usipanic na wala usimuonyeshe kwamba anakutesa.

Assignment na maagizo yote anatoa kwa e mail au kimemo na hataki maswali au ufafanuzi wowote. Sasa hapo kazi itaenda kweli??.
Ukimfata oficn anakupa maelezo huku anaendelea kutazama computer yake as if u r rabbish. Ana maudhi kwa kweli. Dunia hii....
 
kama unafanya kilichokupeleka pale hamna atayekupigia kelele , lakini kama unaendekeza majungu , uvivu , kuwa mtu wa kufuatilia mambo ya watu badala ya kupiga mzigo . lazima ofisi itakuwa chungu.:redfaces:
 
Kaka/dada, we tuliatu, vumilia ndugu yangu, tena we una watoto na nke.tafadhali nakusihi vumilia, mimi binafsi boss wangu ni to much boarin, nasema ukweliiii! alaf ni mmaza, yan anaboa mnooo.lakini sina la kufanya nafanya kazi kwa bidii nipate mtaji wangu, exposure na experience then ntakwit.Umesema hata ukiacha hunapakwenda, hilo linatakiwa kua sababu kubwa ya wewe kutumia busara na hekima ambayo naamini unayo.kamwe usiache kazi kama tu unaona inakulipa no matter wat! as long as interest zako zinatimia waswahili husema funika kaombe mwanharam apite.
 
Show him love, obedience and respect - it will drive HIM CRAZY. Unaweza kushangaa yeye ndo anaweza kukimbia ofisi na kuwaacha nyie mnadunda.

1. Tunza mawasiliano yenu kwa maandishi. Kama mnadiscuss nae kitu, mkimaliza, mtwange email....folloiwng today's discussion etc..

2. Kama anakupa assignment kwa email hakikisha ukimjibu unacopy na wengine ili asijesema hutimizi wajibu wako au kazi yako ilikuwa mbovu

3. Kama anakupatia kazi flani na wakati huo huo unafanya kazi nyingine, mwambie politely kazi unayofanya wakati huo na kama anaridhia uipige chini ili ufanye anayotaka yeye. Kama watu wengine wanasikia, ni poa. Kama hakuna mtu, mtumie email ili kuweka kumbukumbu asije kukugeuka siku za usoni!

4. Be smart, work on agreed targets and meet your deadlines

5. Usipanic na wala usimuonyeshe kwamba anakutesa.

Fuata ushauri huu utakusaidia.
Inakubidi uwe mvumilivu na mwangalifu katika kazi zako. Isije kuwa anataka akufanyie vitimbi ili uache kazi kisha amlete ndugu yake!!
 
Fuata ushauri huu utakusaidia.
Inakubidi uwe mvumilivu na mwangalifu katika kazi zako. Isije kuwa anataka akufanyie vitimbi ili uache kazi kisha amlete ndugu yake!!

He wewe mbona kama vile huyu jamaa unamjua au tupo wote ofisini moja?? Huwezi kuamini tuna branch nchi jirani, wamechishwa kazi mtu na mkewe kwa vitimbi na sasa Jamaa anamprocessia rafiki yake kutoka nnchini kwao viza akajaze ile nafasi..., alikuwa anafanya siri lakini kwenye kikao ikabidi ijadiliwe. Yaani imetuuma kweli coz huyo mtu na mkwewe walikuwa very hardworking na wameondolewa bila kusikilizwa kwa pande zote mbili. Inawezakana ni kampeni yake kutupunguza alete jamaa kutoka nchini mwake. Kweli naapa ntaenda mahakamani wakinifukuza bila sababu.
 
Mwenzenu nimekumbwa na masahibu ambayo najua wengi pia wamepitia sema tunatofautiana uvumilivu na kuhandle stress.

Napiga mzigo kwenye kampuni binafsi bosi mpya wa sasa nae pia mwajiriwa kama sie wengine.Mwanzoni alikuwa mtu wa kawaida kama sisi ila baada ya wakubwa watatu wa juu kuacha kazi, akapandishwa cheo. Ghafla katubadilikia, ni mateso bila chuki na mie sio mvumilivu wa manyanyaso, sema pakwenda sina kozi nina watoto nasomesha na sijapata kwingine.

Naomba msaada wa mawazo, hapa naandika kutoka ofisini, manake jana jioni tumepandishiana kidogo. Yeye anaelewana sana na mkurugnzi nahisi ndio kinachomfanya atunyanyase wenzie. Plz i need ur help kimawazo na how to handle him li isiniafec manake saa nyingine nahisi kuondoka nimwachie ofisi.
Nakikumbuka enzi za utoto nacheka sana............... "MI NIMEKAA TU MWENYEWE KAJA KUNIPIGA".............. sababu za kupandishiana zilikuwa nini............???
Ukifanya kitu gani ndo huwa anakunyanyasa........??
 
Hujawahi kuwa kwenye situation hujui ulilolifanya lakini ghafla kila unalolifanya mwenzio anaona baya na ukimuuliza wat z the problem hupewi jibu la kuridhisha?? Huyu mtu tulikuwa nae dept. moja ila baada ya mabosi watatu kuacha kazi mfulilizo inawezekana labda ni fitina, cheo hicho akapewa yeye.. Sasa wafanyakazi wengine ofisi tunaiona chungu, hata utimize wajibu wako bado report itakayopelekwa kwa wakuu si nzuri.
 
Punguza ku-access JF wakati kazi za watu zinaendelea.....JUST KIDDING

Tafuta maneno haya uyaweke ofisini kwako, kisha yafanyie kazi, niliyakuta kwene ofiisi ya mtu flani ivi, siyakumbuki yote

Dear GOD.... wisdom to understand my boss, courage to adhere to his commands....halafu ikaendeleee lakini ikamalizia hivi... do not give me POWER because I may break his Neck!!! )yatafute uyaweke kwenye ofisi
 
Punguza ku-access JF wakati kazi za watu zinaendelea.....JUST KIDDING

Tafuta maneno haya uyaweke ofisini kwako, kisha yafanyie kazi, niliyakuta kwene ofiisi ya mtu flani ivi, siyakumbuki yote

Dear GOD.... wisdom to understand my boss, courage to adhere to his commands....halafu ikaendeleee lakini ikamalizia hivi... do not give me POWER because I may break his Neck!!! )yatafute uyaweke kwenye ofisi, Weka sehemu ambayo atayaona, utaona atakua mpole!!
 
Nimeshakumbana na mikasa hii wakati nafanya kazi mkoani, bosi wetu alikua binti mmoja hivi mwenye degree ya nutrition, yaani alikua kilaza hakuna mfano, so ili kuficha udhaifu wake akawa mbogo, what I did is, nikawa nafanyakazi smartly na kuweka kumbukumbu, japo alinichafulia sana jina but emails tulizokua tunatumiana zilisaidia sana, tulikua tunajibishana kwenye mails while we"re in da same ofisi and i kept it to my heart, wengine walijua baada ya yy kuzidi kuniponda, nakushauri! mu-ignore tu,
 
Mwenzenu nimekumbwa na masahibu ambayo najua wengi pia wamepitia sema tunatofautiana uvumilivu na kuhandle stress.

Napiga mzigo kwenye kampuni binafsi bosi mpya wa sasa nae pia mwajiriwa kama sie wengine.Mwanzoni alikuwa mtu wa kawaida kama sisi ila baada ya wakubwa watatu wa juu kuacha kazi, akapandishwa cheo. Ghafla katubadilikia, ni mateso bila chuki na mie sio mvumilivu wa manyanyaso, sema pakwenda sina kozi nina watoto nasomesha na sijapata kwingine.

Naomba msaada wa mawazo, hapa naandika kutoka ofisini, manake jana jioni tumepandishiana kidogo. Yeye anaelewana sana na mkurugnzi nahisi ndio kinachomfanya atunyanyase wenzie. Plz i need ur help kimawazo na how to handle him li isiniafec manake saa nyingine nahisi kuondoka nimwachie ofisi.

Pole sana kaka yangu. Mie ya kuajiriwa, na mabosi wakorofi yalinishinda. Maana nilivumilia mpaka yakanifikia kooni. Nikabwaga manyanga. Cha nini kujifia na presha kwa sababu ya kazi za watu....aka, it is not worth it. Mungu si Athuman, nikakutana na coach mzuri wa mafunzo ya biashara................sasa hivi napetaaaa... kuajiriwa sitaki tena!!! Tafuta utaratibu mwingine tu, utapata njia.
 
pole.
Nawe jiangalie huenda una matatizo yako. Nahisi nawe unamdharau kwasababu ulifanyanae kazi katika level yako na sasa yeye amepanda na kuwa kiongozi wako bado wewe unamuona katika level yako.
Usimchukulie poa kwa sababu hiyo na yeye anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa ajira yake mpya.
Vinginevyo fanya kazi kwa bidii acha majungu na ipende kazi yako.
Lastly but important, let the boss be a boss and a leader be so.
 
Punguza ku-access JF wakati kazi za watu zinaendelea.....JUST KIDDING

Bila JF si ndio ofisi ingekuwa chungu kabisa??? angalau nikiingia humu hasira zipungua sema cku akinibamba ndio itakuwa noma. Sema kiswahili kizuri hivi haelewi ndo raha yake.
 
Lazima huyo boss wenu ni mkenya tu ndo wenye tabia hizo, nimefanya nao kazi sana nawaelewa
 
Back
Top Bottom