Mmmmmmh wanwume malaghai sijui kwa nn........?

Mmmmmmh wanwume malaghai sijui kwa nn........?

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Nimshukuru 'Mwenyezi', ndipo yangu nikaanza
Hilo kuacha siwezi, hayupo kunikataza
Muwepo enzi na enzi, wajibu 'kumtukuza'
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Hatumuwezi 'laghai', fani nyingi aziweza
Akikwita hukatai, kwa makini msikiza
Tena yake hukatai, mbio mbio yatimiza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Mbali tenguwa 'katiba', laghai yote aweza
Kwako jifanya swahiba, kumbe vile akubeza
Akaghilibu mahaba, penzi hivi hupoteza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

"Laghai" hana vishindo, mshakia hutoweza
Taratibu wake mwendo, kalimaze zapendeza
Huo ndo wake mtindo, mpaka lake timiza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Tena utacheka nae, hili lile hutowaza
Wendapo kando unae, nyendo zako kichunguza
Ucheke useme nae, mwishowe atakuliza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Matamu yake maneno, hutochoka msikiza
Takuroga kwa mifano, 'mkenge' takuingiza
Kikugubika kwa 'chano', juwa lake kamaliza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Mcheshi hana maringo, ya watu hutosikiza
Utawaona waongo, kumwepuka hotoweza
Takusinga lake singo, kishituka kakuweza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Kwenye ''Siasa'' hakosi, tena huko amekaza
Manenoi pita kiasi, umati akawaweza
"Balozi" hadi "Raisi", njia akawapoteza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

"Uchumi" ndo hamu yake, kukinai hajaweza
Ajaze mifuko yake, ashibe na vya kusaza
Hupanga 'nahau' zake, maneno yakapendeza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

"Utamaduni" sisemi, 'sebene' analiweza
Ukimuona havumi, kume maungo kakaza
Mashughulini hakomi, kila fani jitokeza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

"Laghai" penye wasomi, 'kimombo' hukicharaza
Tena chini hainami, huku kule huangaza
Kwako akitaka kumi, mia utamuongeza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Sio wa kuwa rafiki, tabia kimchunguza
Hahimili kwenye dhiki, mapema 'hujifukuza'
Umwite hakuitiki, hivi atakupuuza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Sijemfanya swahiba, njia atakupoteza
Masikio takuziba, zibuka yasijeweza
Vya kwako akishashiba, huyo akutelekeza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!

Hebu nifike tamati, laghai sawa na kiza
Kikutenda humpati, utaona miujiza
Umfikishe korti, kesi hushinda wa kwanza
Fani nyingi aziweza, 'laghai' hatumuwezi!
 
++ Kaunga njoo huku,,fani ya ushairi hii inakugusa
++
 
Last edited by a moderator:
++ Kaunga njoo huku,,fani ya ushairi hii inakugusa
++

Himidini unafikiri mimi naweza jiita mshairi basi, yaani ni mbabaishaji tu.
Huyu ni another level, maana licha ya vina na mizani kuwa juu hata utajiri wa vocabulary kajaliwa.
 
Last edited by a moderator:
Himidini unafikiri mimi naweza jiita mshairi basi, yaani ni mbabaishaji tu.
Huyu ni another level, maana licha ya vina na mizani kuwa juu hata utajiri wa vocabulary kajaliwa.

++
Kama umemkubali basi tusubiri wengine.
++
 
Himidini unafikiri mimi naweza jiita mshairi basi, yaani ni mbabaishaji tu.
Huyu ni another level, maana licha ya vina na mizani kuwa juu hata utajiri wa vocabulary kajaliwa.

Agreed Kaunga
 
Last edited by a moderator:
Laghai somoye mnafiki, siku zote siwaafiki
Mdomoni ni kama rafiki, moyoni kajaa chuki
Atajifanya shabiki, ukigeuka akuchoma mkuki
Bora nisiwe na rafiki, kujiepusha na mazandiki.

Ninaye collegue kazini, laghai na mnafiki
Huwezi jua awaza nini, tahamaki wapigwa kiki
Kwa majungu hawezekani, tabasamu la plastiki
Nishasema sitaki, urafiki wa mdomoni.
 
tushakuwa malaghai wakati tunawaka mujini ....
 
Laghai somoye chuki,si rafiki asilani
Mna rafiki lukuki,wengine ni majirani
Wananifaa kwa ziki,ningiapo mashakani
Unapopatwa na shida,rafiki huwa hacheki

Sema bado hujajua,sifa za wako rafiki
Ndicho kinokusumbua,kinokutia mikiki
Ni vyema kumtambua,kama sio mnafiki
Rafiki na mnafiki,ndio mtu na somoye
 
Back
Top Bottom