Nadhani tunatumia muda mwingi kujadili matatizo badala ya masuluhisho, unapo sema mzunguko wa fedha mbovu, ama sera mbaya wakati huna uwezo wa kuzibadilisha ni sawa sawa na kupoteza muda na kuibua madonda ya tumbo.
Binafsi na unga mkono hoja wa kufanya Tafiti ya kina sio kwenye kilimo tu la hasha kwenye ujasiliamali wowote ule kwani mambo yanabadirika sana na vile vile ni vyema tukajikita katika kuongeza thamani kwenye mazao ya mashambani mfano unapolima nyanya jaribu kufikiria namna bora ya kuzichakata kwavyo ukiwa umezifanyia packaging no rahisi sana kaka perishable product kukaa muda mrefu.
Kwenye huo mfano wa nyanya mathalani mwaka jana kulikua na mwamko mkubwa wa kilimo cha nyanya hivyo mazao yalikuwa mengi sana lakini factor ya demand bado tuliendelea kutegemea traditional market ile ile sasa kwa mtu aliyefanya Tafiti ya kutosha agharabu angeweza kufanya usindikaji wa hizo nyanya ambayo ni very cheap and simple technology lakini hata kama angekuwa na changamoto za kutokuwa na maarifa ya kusini kusindika na endapo a alifanya tafiti ya mnyororo wa thamani wa zao analotaka kupanda basi angeweza kufahamu kwamba demand ya nyanya haikuwa equally distributed nchini mwetu achilia mbali issue ya export market hivyo angefahamau kwamba wakati kuna ziada ya uzalishaji mathalani Morogoro bado shinyanga kulikua na demand kubwa hivyo kama angewekeza vizuri katika tafiti yake angekuwa na njia ya kusafirisha na namna bora ya kuwafikia wateja wake.
Ushauri wangu wa jumla tuache kulalamika na kutumia muda mwingi kujadili matatizo badala ya majawabu.
fungolee@gmail.com
0714 764 589