Mliwaweka gerezani bila hatia, mmewekwa karantini bila kujali vyeo vyenu

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Wapo wapo hawana hatia wapo magerezani kwa sababu mtu fulani ameelekeza iwe hivyo. Wakati tunawaweka magerezani tuliamini tutakuwa huru na hatutakufa kabla yao. Sisi tunaojiona tupo huru tumewekwa karantini na hatuna Uhuru wa kutembea tupendavyo.

Baadhi ya waliowaweka gerezani wametangulia mbele ya haki na wale waliopo magerezani ipo siku watatoka na kuishi uraia wakati karantini imeisha.

Tulitamani watoto wao wakose ada na wasiendelee na masomo, ila sasa hata watoto wenu wapo nyumbani kama walivyo watoto wao.

Mlikataza watu kwenda kuwasalimia magerezani mkawagombanisha na kuwaogofya watu wasitoe msaada wowote kwao. Leo hakuna anayekuja majumbani kwenu, mmebaki kama yatima kwa kuogopo wageni.

Mlituaminisha kwamba wao waliomagerezani siyo wazalendo na hawaitakii mema Tanzania, leo mmetutenga na kila mmoja wenu anatetea nafsi yake ipate kuishi.

Mwenyenzi Mungu anatoa adhabu kwa haki ninyi mnatoa adhabu kwa kuyatumia madaraka mliyopewa vibaya. Msihukumu nanyi amtohukumiwa, mnaowatesa kwa kuwaweka ndani Wana amani kulipo ninyi mlio huru mtaani.
 
Tumejiweka retensheni wenyewe vijijini kwetu kama enzi za Mwalimu ukienda kinyume na serikali yake. Kweli Mungu fundi.
 
Na bado sana, hiki kizuizi kinaendelea sana kwa sababu kirusi hiki ndo kwanza kinashika kasi, kizuizi hiki ni zaidi ya cha kina Rugemalila. Wale vijana wa human rights na wengineo, hata wasiopenda kuvaa barakoa watazivaa tu muda ukifika hahahah Mungu fundi kweli, corona the equalizer

Sent using Jamii Forums mobile app
 
teh! teh! teh! Karma!

Halafu pamoja na dhulma na madhambi yote ya wazi wazi kwa wadanganyika lakini bado kuhami mkuu bila hata aibu anahudhuria ibada tena anakaa siti ya mbele, anapenda kutumia kamsemo kake, "Msema kweli ni mpenzi wa Mung"

Huyu jamaa ikatokea nikamkuta peponi namzaba kibao mbele ya malaika wa zamu
 
Hii inafikirisha sana. nameipenda hii kutoka kwa mdau hapo juu "Corona the equalizer"
 
teh! teh! teh! Karma!

Halafu pamoja na dhulma na madhambi yote ya wazi wazi kwa wadanganyika lakini bado kuhami mkuu bila hata aibu anahudhuria ibada tena anakaa siti ya mbele, anapenda kutumia kamsemo kake, "Msema kweli ni mpenzi wa Mung"

Huyu jamaa ikatokea nikamkuta peponi namzaba kibao mbele ya malaika wa zamu
😁😁😁😁🤣😂🤣
Mbinguni hakuna fujo na pia yote ya duniani yanasahaulika. Kwa hiyo huwezi kukumbka chochote.
 
Back
Top Bottom