Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
MLIVUTA BANGI ?
1)Mlifanya ukatili,adhabu ni haki yenu.
Mlitenda ubatili,mkazika ndoto zenu.
Ulikuwa ujahili,mwajua taluma yenu ?
Hivi mlivuta bangi ?.
2)Mmeshakuwa mgambo,kuyatembeza mangumi.
Sasa namchapwe fimbo,mkajifiche mikumi.
Harobaini ni fumbo,zenu tena siyo kumi.
Hivi mlivuta bangi ?
3)walimu ni taaluma,vipi mwaidhalilisha.
Ni nani alowatuma,mkapata kujishusha.
Japo kweli inauma,tena mmejiangusha.
Hivi mlivuta bangi ?.
4)ualimu na hasira,kama tembo na bahari.
Hivi hamjui dira,ama mlisha kariri.
Kama nyoka mkafura,mkavimba kama ngiri.
Hivi mlivuta bangi ?.
5)mnamkabia chini,kwani jambazi a mwizi.
Na makofi ya usoni, kama mnavunja nazi
Waziri wa wizarani,sasa kawafuta kazi.
Hivi mlivuta bangi ?
6)wambieni na wengine,shuleni wawe makini.
Msije siku nyingine,mkashia mtaani.
Na wananchi wengine,wa sheria mkononi.
Hivi mlivuta bangi ?
Shairi= MLIVUTA BANGI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+25562401016.
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
1)Mlifanya ukatili,adhabu ni haki yenu.
Mlitenda ubatili,mkazika ndoto zenu.
Ulikuwa ujahili,mwajua taluma yenu ?
Hivi mlivuta bangi ?.
2)Mmeshakuwa mgambo,kuyatembeza mangumi.
Sasa namchapwe fimbo,mkajifiche mikumi.
Harobaini ni fumbo,zenu tena siyo kumi.
Hivi mlivuta bangi ?
3)walimu ni taaluma,vipi mwaidhalilisha.
Ni nani alowatuma,mkapata kujishusha.
Japo kweli inauma,tena mmejiangusha.
Hivi mlivuta bangi ?.
4)ualimu na hasira,kama tembo na bahari.
Hivi hamjui dira,ama mlisha kariri.
Kama nyoka mkafura,mkavimba kama ngiri.
Hivi mlivuta bangi ?.
5)mnamkabia chini,kwani jambazi a mwizi.
Na makofi ya usoni, kama mnavunja nazi
Waziri wa wizarani,sasa kawafuta kazi.
Hivi mlivuta bangi ?
6)wambieni na wengine,shuleni wawe makini.
Msije siku nyingine,mkashia mtaani.
Na wananchi wengine,wa sheria mkononi.
Hivi mlivuta bangi ?
Shairi= MLIVUTA BANGI.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+25562401016.
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.