MLIPUKO WA BARUTI KWENYE MAKAZI

MLIPUKO WA BARUTI KWENYE MAKAZI

kitoromondo

Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
64
Reaction score
75
BARUTI HOLELA KWENYE MAKAZI, ndugu wana jukwaa, naomba kutumia jukwaa hili teule kwa anaye husika atusaidie mimi na wakazi wenzangu wa KIGALA kata ya BUSWELU wilayani ILEMELA, kumekua ulipuaji wa baruti hapa mtaani majira ya saa 10:00am hadi saa 3:00pm ,hii ni kwa muda wa miaka zaidi ya mitatu sasa ,mtu huyu anaefanya ulipuaji huu anajulikana, anadai ana KIBALI toka wizarani kuwa anatafuta MALIKALE ,ni katika eneo analoishi, mtu huyu amekua ni KERO kwa baruti na matetemeko yatokanayo na ulipuaji huo ,Mwenyekiti wa serikali ya mtaa anajua, mtendaji kata ya Buswelu anajua pia mh diwani anafamu lkn sisi wakazi tunateseka ,Iweje serikali hii ya sisi wanyonge ,iruhusu hili kufanyika kwenye makazi ya wananchi? Ni Mali Kale gani inatafutwa kwa BARUTI zaidi ya miaka mitatu?Serikali yangu na wahusika, hapa kuna zaidi ya MALI KALE, na Hii milipuko inatuletea taharuki kubwa, japo madhara kiafya na nyumba zetu hatuyajui.
 
Jiongezeni muende kwa mbunge wenu,mkuu wa wilaya mpaka kwa mkuu wa mkoa
 
Back
Top Bottom