tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,854
Viongozi mliotimuliwa CHADEMA aacheni malumbano yasiyo na tija. Kama ni demokrasia, CHADEMA ndiko iliko demokrasia ya kweli.
1. Viongozi wa Chadema waliwaonesha Demokrasia ya Kweli kwa kuwavumilia kisiasa kwa muda mrefu, sasa wameamua kutenda kazi yao kama Viongozi wanaosimamia kanuni, sheria na uwajibikaji.
2. Kanuni na taratibu za rufaa zipo, kateni rufaa kwa sababu ni haki yenu na utaratibu kidemokrasia katika Chadema na Katiba ya Nchi.
3. Maoni ya Zitto Kabwe, ni maoni na haki yake kidemokrasia katika kutoa maoni yake kama mwanachama huru. Pia sisi raia tuna haki ya kusikiliza na kukubaliana nae au kutokubaliana nae kidemokrasia. Chadema ni Chama cha Demokrasia kinachoundwa na watu na sio mtu.
3. Kuhusu Viongozi wa juu wa Chadema kuchukua fedha kutoka ktk chama isiwe ndiyo agenda pekee inayosimamia malalamiko ya kufukuzwa kwenu. Kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa, hakuna jinai wala uvunjanji wa sheria yoyote ya nchi, kwa mtumishi wa Taasisi, Chama, Asasi, au Kampuni, kukopa fedha kihalali kwa ajili ya maendeleo yake kimaisha. Ikumbukwe kuwa Viongozi wa Chama ni binadamu kama walivyo binadamu wengine na wanazo haki na stahili za kukopa na kukopeshwa kihalali kwa mujibu wa sheria kama raia na mwajiliwa mwingine yeyote. Mbaya ni ufisadi na wizi wa mali na rasimali za umma na Taifa.
4. Kulalamika kwenu kumekuja kipindi ambacho mko katika harakati za kuondolewa katika chama, je, mlikuwa wapi hapo awali? Mimi nawashauri Mkate rufaa kama ilivyo kidemokrasia katika kanuni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Vinginevyo malalamiko yenu yataonekana kama sehemu ya hasira na kisasi baada ya kutimuliwa.
NI USHAURI TU, MSIJENGE CHUKI.