Mliomuibia mdogo wangu magunia 70 ya mahindi Singida rudisheni tafadhali

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Salaam kwenu japo sitamani wahusika watukio hili waitikie Salam yangu.

Uuzaji wa nafaka ni moja Kati ya harakati ninazozifanya ili kuutafuta mkate wangu wakila siku.

Huwa nasafirisha mahindi kutoka hapa mkoani kwangu kwenda mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Singida.

Wiki iliyopita nikawa sipo vizuri kiafya hivyo nikamuomba mdogo wangu anisaidie kupeleka mzigo Singida.Yalikua magunia 70 yamahindi ambapo Kuna mteja nilipatana nae kumpelekea.

Dogo anadai alifika na mzigo salama, akapakua na gari iliyoyabeba ikajiondokea zake akabaki yeye na mzigo.

Kwa kuwa muda Ulikua umeenda akaona aende kulala gesti jirani na alipopakulia mzigo. Katika Hali ya kushangaza hakukabidhi mzigo kwa mtu yeyote na aliamini asubuhi atakuta mzigo wake Kama alivyouweka.

Asubuhi anaenda kucheki mzigo anakuta patupu, hakuna hata alama kuonyesha kulikua na magunia70 ya mahindi eneo hilo.

Hapa nimechanganyikiwa kwani nahisi Kama sio uzembe basi Kuna kamchezo dogo kanichezea.

Amenipigia simu kunieleza hayo huku akionekana na yeye kachanganyikiwa kwani anauliza "broo nirudi huko nyumban utanisamehe au nitafute tu pakwenda?"

Nimemwambia aendelee kuulizia labda atapata fununu yahayo mahindi yalipo.Wakati anaendelea kuyatafuta naomba mnisaidie;Huyu dogo atafute pakwenda Kama alivyoomba au nimwambie arudi nyumbani nilipo.
Kama nihasara nimeipata yakutosha wakuu.

Wasalaam!
 
Dogo kakuliza kapata mtaji unawezaje kuacha mzigo bila makubaliano
 
Singida namfua kuna walinzi unawapa buku mbili wanakupa mzigo asubuhi, wakati huu wa njaa analala gesti na mzigo hajakabidhi mtu wala mwenyeji kuja kuuona mzigo, dogo ni bwege kiufupi
 
Sioni kama unataka msaada wa kumjua mwizi, zaidi ya kuomba ushauri juu ya hatma ya dogo..
 
Mahindi sasa hivi gunia moja la kilo 100 ni 80,000 kwahio kuna mawili hapo ni kweli kaamua kukupiga changa la macho, au wahuni walimsoma wakajua dogo ni mshamba wakamsoma ramani wakamuibia...
🤔🤔 Gunia 70 zinaibiwa vipi..?
 
Yule demu aliyelala naye guest wakiwa wamelewa anajua mchezo wote. Dogo arudi tu home.
 
Salaam kwenu japo sitamani wahusika watukio hili waitikie Salam yangu.

Uuzaji wa nafaka ni moja Kati ya harakati ninazozifanya ili kuutafuta mkate wangu wakila siku.

Huwa nasafirisha mahindi kutoka hapa mkoani kwangu kwenda mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Singida.

Wiki iliyopita nikawa sipo vizuri kiafya hivyo nikamuomba mdogo wangu anisaidie kupeleka mzigo Singida.Yalikua magunia 70 yamahindi ambapo Kuna mteja nilipatana nae kumpelekea.

Dogo anadai alifika na mzigo salama, akapakua na gari iliyoyabeba ikajiondokea zake akabaki yeye na mzigo.

Kwa kuwa muda Ulikua umeenda akaona aende kulala gesti jirani na alipopakulia mzigo. Katika Hali ya kushangaza hakukabidhi mzigo kwa mtu yeyote na aliamini asubuhi atakuta mzigo wake Kama alivyouweka.

Asubuhi anaenda kucheki mzigo anakuta patupu, hakuna hata alama kuonyesha kulikua na magunia70 ya mahindi eneo hilo.

Hapa nimechanganyikiwa kwani nahisi Kama sio uzembe basi Kuna kamchezo dogo kanichezea.

Amenipigia simu kunieleza hayo huku akionekana na yeye kachanganyikiwa kwani anauliza "broo nirudi huko nyumban utanisamehe au nitafute tu pakwenda?"

Nimemwambia aendelee kuulizia labda atapata fununu yahayo mahindi yalipo.Wakati anaendelea kuyatafuta naomba mnisaidie;Huyu dogo atafute pakwenda Kama alivyoomba au nimwambie arudi nyumbani nilipo.
Kama nihasara nimeipata yakutosha wakuu.

Wasalaam!
Huyo dogo Kuna namna,unawezaje kuacha mzigo kama huo bila ulinzi? Na kwanini akuulize atafute pa kwenda? Mwambie arudi nyumbani ili umjambishe
 
Twende taratibu,kumbuka naandika maelezo hapa na baadae yaweza kuwa ushahidi mahakamani!
1.Kwahiyo wakati unampatia mzigo ulishafahamu juu ya uwezo wake wa kusafiri sehemu za mbali na nyumbani?
2.Je,wakati unampatia mzigo ulisahau kumwambia wapi/stoo gani utahifadhiwa ama nani atampokea?
3.siku zote ukisafirisha wewe huwa unauza jumla au rejareja popote barabarani?
Nitaendelea ukishajibu haya!
 
Back
Top Bottom