Mliojiandikisha BVR UDSM, Mnahakiki wapi taarifa zenu?!

Goodluck Mshana

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,271
1,119
Kwa wale ambao mlipata fursa ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kwa njia ya BVR pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni wapi mnahakiki taarifa zenu?! Hasa kwa wale walijiandikisha kwenye vituo vya Cafeteria, Nkuruma na Mlimani Primary.

Nauliza maana kituo changu kilikuwa pale Cafeteria. Jana nimefika sijakuta dalili zozote za uhakiki huo kufanyika!!! Naombeni msaada haraka maana muda umeyoyoma sana kwa wakazi wa Dar kuhakiki.

Labda pia nijazie hapa. Nimejaribu mfumo wa ki electronic wa NEC kwa kuingiza namba za kadi yangu kupitia namba *152*00# na kwenye web yao www.voters.nec.go.tz. Kote huko inaonekana SIJAJIANDIKISHA.!!! Huu niuite ni UHUNI uliokubuhu wa Tume. Zile fingerprint na taarifa zetu mmepeleka wapi?

Kwa mchezo huu hakika tutapigana VITA MAPEMA ASUBUHI. Natoa Rai kwa Tume ya Uchaguzi kuwaacha watanzania WOTE waliojiandikisha wakapige kura hiyo October 25. Vinginevyo mtaitia kiberiti hii nchi.

Uhakiki ni process ngumu na ndefu. Zoezi hili linahitaji muda na umakini kwa wahusika (IT personnel). Siyo jambo la kukurupuka na kutaka kutimiza azma za kisiasa. Nasema Tume ya Uchaguzi itangulie The Hague na kuanza mazoezi ya jela.

Kwa mwenye taarifa TAFADHALI


Asanteni.
 
Lakini pia tumia cellular yako kwa kubonyeza *152*00# then fuata maelekezo.
 
Kazi ya uhakiki ni ya tume yenyewe, jukumu letu sisi sote wenye vitambulisho ni kupiga kura tu
 
NEC wasikwepe majukumu yao... Wanatakiwa wahakiki majina ya wote waliopewa vitambulisho....

Mnatafuta pa kujihakikia kwani hiyo ni kazi yenu.... nauliza ni kazi yenu...?? Au hivyo vitambulisho/kadi mlipewa na taasisi nyingine tofauti na NEC...??

Ninachoamini.... Kila mwenye kitambulisho/kadi atapiga kura... Make hatutatumia teknolojia ya BVR/BVID kupiga kura... Kila kitu ni analogia.
So kila mwenye kitambulisho/kadi anayo haki ya msingi kabisa kupiga kura yake tarehe 25/10/2015 (PERIOD)!
 
Wakuu hamna hajavya kutafuta kituo, wewe tumia njia za kidigitali inatosha kujua kama data zako ziko kwenye database yao! kuna njia mbili

1. PIGA *152*00# kisha fata maelekezo yako straight forward!
2.Ingoa kwenye link ya nec voters.nec.go.tz:8081/vote kisha fuata maelekezo
 
Lakini pia tumia cellular yako kwa kubonyeza *152*00# then fuata maelekezo.

Mwisho wa yote hiyo namba haina msaada wowote; wanakwambia... Kuhakiki kitambulisho cha mpira kura - fika kwenye kituo cha uandikishaji...
Nikafanye nini wakati nilishajiandikisha...
Kazi yangu ni moja tu sasa... K.U.P.I.G.A K.U.R.A!
 
Wakuu hamna hajavya kutafuta kituo, wewe tumia njia za kidigitali inatosha kujua kama data zako ziko kwenye database yao! kuna njia mbili

1. PIGA *152*00# kisha fata maelekezo yako straight forward!
2.Ingoa kwenye link ya nec voters.nec.go.tz:8081/vote kisha fuata maelekezo

Huko kote nimepita mkuu... Taarifa wanayonipa ni kwamba SIJAJIANDIKISHA...
 
Yawezekana mimi wananielewa ndiyo maana hawanipi maelezo hayo mkuu. Baadaya ya hiyo namba kuna sehemu naulizwa nijaze namba ya kitambukisho changu then narudishwa details za wapi nikijiandikisha na kila kilichohusika siku ile nilipojiandikisha.

Sasa kama wewe Jp Omuga wanakupa positive details wanadhani ni #UKAWA so inakula kwako.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom