Mliofanya interview tume ya ajira tar 19/20 june 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mliofanya interview tume ya ajira tar 19/20 june 2012

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by salosalo, Jun 22, 2012.

 1. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Sitaki kuamini kwamba JF haukuwa na muwakilishi hata mmoja kwenye interview ya tar 19 na 20 June, ikiwa ulihudhuria sema japo kwa kifupi ukiongozwa na maswali mawili yafuatayo;
  1. swali gani la ufahamu ambalo unahisi hukujibu sawa? liseme upate mwongozo kwaajiri ya kesho.
  2. umejifunza nini kutokana na interview yako nasi unatufundisha nini?
  funguka ili tuwasaidie na wengine ama wasifanye makosa kama yako kesho au waivae interview kwa ushindi kama wewe

  Kumbuka:
  Ni muhimu kujitathimini kila baada ya interview
  usipopata kazi, mara zote haimaanishi ulikosea kwenye interview. wakati mwingine wote mkifanya vizuri basi bahati huchukua nafasi 7bu nafasi ni chache.
   
 2. DullyJr

  DullyJr JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,039
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Nini UDHAIFU na uimara wako kiujumla?
   
 3. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  katika kukabiri swali kama hili unatakiwa kiwa makini sana. kwanza inabidi uwe umeandaa majibu
  ya swali kama hili mapema(hutakiwi kuchukua muda mrefu kufikiri ili kujibu swali kama hili, vinginevyo itaashiria unatunga majibu na kwamba hujifahamu vizuri wewe mwenyewe:

  sasa natuanze na uimara wako.
  siku zote kile kile kinachomfanya mtu kuitwa bora kuliko mwingine ndio uimara wake. pia kumbuka uimara wa mtu hubadilika kutegemeana na kazi au eneo la kazi. namaanisha ukatiri ni uimala wa mtu aombaye kazi ya jeshi, lakini ni udhaifu kwa aombaye kazi ya udactari(ni mfano tu)

  ili kujibu vizuri uimara wako, fanya yafuatayo kabla ya kwenda kwenye interview
  1. soma mahitaji ya uwezo binafsi unaotakiwa mbali na taaluma ya darasani maana wote mtakuwa nayo. basi hapo ndipo unapotakiwa kuundia uimara wako. mfano anatakiwa mtu mwaminifu, mchangamfu,mwenye kujisimamia kazi,uwezo wa kuongoza au kuanzisha mahusiano kirahisi
  2. kama hawakuandika kwenye tangazo, basi fikiria mambo ya pekee ambayo mtu wa nafasi hiyo anapaswa kuwa nayo nje ya elimu ya darasani.
  3. epuka kutaja uimara wako moja kwa moja kama: mimi ni mwaninifu, mimi ni mchapa kazi sana. ninauwezo wa kufanya kazi zaidi ya moja kwa muda mmoja n.k HAIFAI KABISAA TENA NASEMA HAIFAI. Taja uimara wako kwa kuelezea matukio yaliyo kupelekea kutambulika kuwa na uimara huo na si vinginevyo. mfano, anaweza ukasema hivi: mwaka 2000 nilipewa dhamana ya kusimamia fedha za miradi wa ujenzi mara baada ya kurejesha pesa nilizo okota baada ya mhasibu kupoteza. wakati wa kupewa dhamana hiyo niliambiwa uaminifu wangu ndio ulionipa nafasi hiyo. au anza hivi: tangu nikisoma nimekuwa mtu wa kupigania kufikia malengo ya kwenda shule amboyo yaliikuwa ni kufaulu masomo na kweli nilifaulu kwa kila hatua. mpaka leo dhamira ya kufanikisha malengo niliyojiwekea au kuwekewa ni ya lazima niwapo kazini. Au sema hivi: nimejifunza vitu vingi vipya nikiwa ....(TBL) kama ....., ......., ....., na ......... vingine sijapata kuvitumia popote hadi leo, ila vilivyo vingi ndo vimenipa cheo pale Cocacola Co.hata sijui ilikuwaje nikaweza kujifunza vitu vingi kwa haraka namna hiyo. n.k
  4. Vyovyote utakavyojibu Ndugu ni sawa ila kumbuka kuweka viambatanisho,yaani usiwape mifupa bila nyama
  5. Pia unapokuwa kwenye interview, kumbuka kujieleza kwa namna ambayo wasilikiliza watavutiwa kukusikiliza. Kila wanapokuuliza swali chukulia kuwa kweli hawajui na wewe ndo unatakiwa kuwajuza kwa muda mfupi sana ila kwa namna ambayo hawatakusahau kirahisi hata baada ya watu kumi watakaofuata.

  Kwa leo tuishie hapa, Namna ya kujibu udhaifu wako itafuata baada ya kujiridhisha kwamba hii ya kwanza imeeleweka. tafadhali iliza popote unapodhani hapajaeleweka
   
 4. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  jibu swali acha hoja eti sijui nini
   
 5. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  tena hujui tu kuwa wewe ndo unasababisha na wengine wasubiri ili kukungoja wewe unaechelewa kuelewa. Hiyo post ya kwanza tu hujaelewa,je ningeweka yote si ningekupoteza kabisa wewee? Zingatia na elewa hii "Kwa leo tuishie hapa, Namna ya kujibu udhaifu wako itafuata baada ya kujiridhisha kwamba hii ya kwanza imeeleweka. tafadhali iliza popote unapodhani hapajaeleweka" na hapo usipoelewa Itabidi nianzishe crush program maalumu kwako:dance:
   
 6. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  bado unachemka umeulizwa swali si useme hujui...siitaji hivyo vi interview koko. mie nimejibu tu kutokana na maandishi yako mwenyewe ya ulivyomjibu mwenzetu alichokuuliza,
  ndio niliposoma hayo mengine macho yariruka as mie ni mmoja wa wasio soma yote kama nimeona sina interest na thread iliyorushwa.
   
 7. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  pole sana
   
 8. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Eti udhaifu utafata, unapenda kuwa lecturer eeh? We mwaga manondo hayo mwanzo mwisho, hatuko kipind cha watoto cha redioni, umeandaa maelezo then ni busara kuelezea yote TUKIPOTEZA SIMU AU 2KIKOSA ELA YA NET AU MALAPTOP YAKIBUMA? ACHA HIZO MTOA MADA.
   
 9. DullyJr

  DullyJr JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,039
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  umeeleweka kaka,twende katika udhaifu kwani hapo ndipo haswaa panapotatiza
   
 10. F

  Fhiza New Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello....Umesomeka asante....
   
 11. t

  tara Senior Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tuendelee kumsubiria atarudi tu.....
   
 12. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Sasa naomba turudi kwenye mwendelezo wetu wa swali la interview. Leo ni jinsi ya kuelezea udhaifu. Kumbuka kwamba watu husema kulijua tatizo ni hatua kubwa kuelekea ufumbuzi wa tatizo hilo au pia husema ukimjua adui basi huyo si adui tena.

  • Wakati unaelezea udhaifu usisahau kuwa udhaifu ni tatizo, hivyo kama unajua udhaifu ulionao basi wewe ni dhaifu sana maana unajua tatizo na unaliacha liendelee kukua(mwajiri atajua ndivyo utakavyofanya kwa madhaifu utakayo kumbana nayo kazini pindi akikuajiri)
  • Wakati wote taja udhaifu katika hali ya wakati uliopita na uonyeshe kwamba kwa sasa si sehemu ya udhaifu huku ukijaribu kuelezea jinsi ulivyo ondokana na udhaifu huo.
  • Upuka tena epuka kabisaa kutaja udhaifu wako moja kwa moja maana hiyo itamaanisha uwapo kazini utakuwa ukiyasema na kuyaweka wazi madhaifu ya mwajiri wako.
  • Duniani hamna ntu asiye na madhaifu, hivyo usidhubutu kusema huna madhaifu na pia utajapo madhaifu yako jaribu kutaja kwa kifupi kadri uwezavyo,lakini ukieleweka.
  • Tafadhali sana jitahidi kutoa majibu yenye uhalisia nay a kweli kwa kila mwenye ufahamu,vinginevyo utakuwa unaonyesha udhaifu wako mkubwa bila kujijua. Mfano utaonyesha kuwa wewe ni Muongo,si mwaminifu, unakiburi, usiye na malengo n.k

  MFANO WA UDHAIFU:
  Anza kujibu swali la udhaifu kwa namna yoyote inayofanana nahii:
  Udahifu wowote ule ni sehemu ya tatizo ama kazini au katika maisha ya kawaida katika jamii, hivyo matatizo niliyowahi kukumbana nayo katika maisha yalinisaidia kubaini madhaifu yangu na kutafuta ufumbuzi wake mara moja ama kwa kufundishwa darasani, kufundishwa na rafiki au kujisomea mwenyewe:-

  1. Sina uwezo wa kupangilia na kutekeleza kazi zinapokuwa nyingi kwa kufuata umuhimu wake isipokuwa kwa kuziorodhesha kwa kufuata umuhimu na baadaye kukamilisha moja baada ya nyingine huku nikizingatia muda
  2. Mpaka sasa niko kwenye mafunzo ya jinsi ya kutumia computer katika kozi ambayo nahudhuria kila jioni. Hii ilikuja baada ya kugundua kuwa nimeachwa nyuma na hii teknologia mpya. Kwa sasa report zangu za kazini zote natengeneza kwa kutumia komputa
  3. Bosi wangu niliyefanya nae kazi kwa mara ya kwanza alinifundisha namna ya kuchukua maelekezo na kuyafanyia kazi. Hapo kabla sikuwa na uwezo huo. Nilikuwa nikihudhuria vikao na mikutano kama kukamilisha ratiba. Kwa sasa siko hivyo tena
  4. Mimi nimekuwa msahaulifu sana wa matukio yanayotegemewa kutekelezwa siku za mbele kwa makubaliano ya leo. Hata hivyo rafiki yangu alinifundisha kukumbuka kila kitu kwa kuandika matukio yote kwenye kalenda. Kila siku kabla ya kuondoka kazini naandaa mpango kazi wa siku inayofuata
  5. Sina uwezo wa kuona mbali kwa macho ya kawaida jambo ambalo limenifanya niende hospitali na kupewa miwani ambayo imeondoa tatizo hilo kwa asiliamia mia.

  Wengine hupenda kugeuza uimara uliopitiliza kuwa kama ndio udhaifu wao. Kama kusema :nakosa raha sana nikishindwa kufikia malengo, sipendi kushindwa kitu kirahisi, mimi ninahuruma iliyopitiliza, sijui kumchukia au kukosana na mtu. Aina hii ya udhaifu inaonyesha udhaifu mkubwa ulionao kupitia kila unalosema. Hii ni kwa sababu kila kitu kizuri kinapokosa kiasi basi huwa kinakuwa na madhara makubwa kuliko hata ubora wake. Mfano ni Madhala ya gari. Ni zuri sana maana liendapo kasi linatufikisha haraka tuendako lakini lizidisha mwendo sio kwamba hatufiki tu kule tulikotaka kuwahi bali pia tunapoteza maisha, mali, na kusababisha huzuni, taabu na gharama kwa waliobaki. Hebu pima hasara ya gari ikitumiwa vibaya dhidi ya faida kama ikitumika vema. Kwa vyovyote hasara ni zaidi ya faida .
   
 13. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Sasa naomba turudi kwenye mwendelezo wetu wa swali la interview. Leo ni jinsi ya kuelezea udhaifu. Kumbuka kwamba watu husema kulijua tatizo ni hatua kubwa kuelekea ufumbuzi wa tatizo hilo au pia husema ukimjua adui basi huyo si adui tena.

  • Wakati unaelezea udhaifu usisahau kuwa udhaifu ni tatizo, hivyo kama unajua udhaifu ulionao basi wewe ni dhaifu sana maana unajua tatizo na unaliacha liendelee kukua(mwajiri atajua ndivyo utakavyofanya kwa madhaifu utakayo kumbana nayo kazini pindi akikuajiri)
  • Wakati wote taja udhaifu katika hali ya wakati uliopita na uonyeshe kwamba kwa sasa si sehemu ya udhaifu huku ukijaribu kuelezea jinsi ulivyo ondokana na udhaifu huo.
  • Upuka tena epuka kabisaa kutaja udhaifu wako moja kwa moja maana hiyo itamaanisha uwapo kazini utakuwa ukiyasema na kuyaweka wazi madhaifu ya mwajiri wako.
  • Duniani hamna ntu asiye na madhaifu, hivyo usidhubutu kusema huna madhaifu na pia utajapo madhaifu yako jaribu kutaja kwa kifupi kadri uwezavyo,lakini ukieleweka.
  • Tafadhali sana jitahidi kutoa majibu yenye uhalisia nay a kweli kwa kila mwenye ufahamu,vinginevyo utakuwa unaonyesha udhaifu wako mkubwa bila kujijua. Mfano utaonyesha kuwa wewe ni Muongo,si mwaminifu, unakiburi, usiye na malengo n.k

  MFANO WA UDHAIFU:
  Anza kujibu swali la udhaifu kwa namna yoyote inayofanana nahii:
  Udahifu wowote ule ni sehemu ya tatizo ama kazini au katika maisha ya kawaida katika jamii, hivyo matatizo niliyowahi kukumbana nayo katika maisha yalinisaidia kubaini madhaifu yangu na kutafuta ufumbuzi wake mara moja ama kwa kufundishwa darasani, kufundishwa na rafiki au kujisomea mwenyewe:-  1. Sina uwezo wa kupangilia na kutekeleza kazi zinapokuwa nyingi kwa kufuata umuhimu wake isipokuwa kwa kuziorodhesha kwa kufuata umuhimu na baadaye kukamilisha moja baada ya nyingine huku nikizingatia muda
  2. Mpaka sasa niko kwenye mafunzo ya jinsi ya kutumia computer katika kozi ambayo nahudhuria kila jioni. Hii ilikuja baada ya kugundua kuwa nimeachwa nyuma na hii teknologia mpya. Kwa sasa report zangu za kazini zote natengeneza kwa kutumia komputa
  3. Bosi wangu niliyefanya nae kazi kwa mara ya kwanza alinifundisha namna ya kuchukua maelekezo na kuyafanyia kazi. Hapo kabla sikuwa na uwezo huo. Nilikuwa nikihudhuria vikao na mikutano kama kukamilisha ratiba. Kwa sasa siko hivyo tena
  4. Mimi nimekuwa msahaulifu sana wa matukio yanayotegemewa kutekelezwa siku za mbele kwa makubaliano ya leo. Hata hivyo rafiki yangu alinifundisha kukumbuka kila kitu kwa kuandika matukio yote kwenye kalenda. Kila siku kabla ya kuondoka kazini naandaa mpango kazi wa siku inayofuata
  5. Sina uwezo wa kuona mbali kwa macho ya kawaida jambo ambalo limenifanya niende hospitali na kupewa miwani ambayo imeondoa tatizo hilo kwa asiliamia mia.

  Wengine hupenda kugeuza uimara uliopitiliza kuwa kama ndio udhaifu wao. Kama kusema :nakosa raha sana nikishindwa kufikia malengo, sipendi kushindwa kitu kirahisi, mimi ninahuruma iliyopitiliza, sijui kumchukia au kukosana na mtu. Aina hii ya udhaifu inaonyesha udhaifu mkubwa ulionao kupitia kila unalosema. Hii ni kwa sababu kila kitu kizuri kinapokosa kiasi basi huwa kinakuwa na madhara makubwa kuliko hata ubora wake. Mfano ni Madhala ya gari. Ni zuri sana maana liendapo kasi linatufikisha haraka tuendako lakini lizidisha mwendo sio kwamba hatufiki tu kule tulikotaka kuwahi bali pia tunapoteza maisha, mali, na kusababisha huzuni, taabu na gharama kwa waliobaki. Hebu pima hasara ya gari ikitumiwa vibaya dhidi ya faida kama ikitumika vema. Kwa vyovyote hasara ni zaidi ya faida .:dance:
   
 14. Y

  YOSAYOSA Member

  #14
  Jun 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya mkubwa
   
 15. ICHANA

  ICHANA JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,808
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  :focus:thanx kwa maelezo yko
   
Loading...