Mlio mbaya kwenye gari

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
1,845
2,247
Habari wakuu.
Nina gari yangu ndogo ninapowasha inatoa mlio mbaya sana kama mashine za kusaga nafaka zile za zamani na inawaka kwa shida mpaka nikanyage mafuta huku nawasha.
Lkn ikiwaka baada ya muda kidogo inatulia.
Msaada wakuu.
 
Hapana mkuu haiwaki
Gaira aina gani hio?

Mkuu kama unasikia mlio kama chuma kinagonga chuma mwenzake kama vile kugonga hodi kwa haraka katika mlango basi hio ni engine knock, usitembelee gari hio. Tega sikio lako karibia engine, sikiliza mlio unatoka wapi, yawezekana ni milio inatoka sehemu za pulley za kuzungushia belt ya alternator, compressor, timing n.k kama ukisikia sehemu izo, jaribu kutafuta DW-D40 upulizie kwenye hizo pulley kisha sikiliza kama inaendelea.
 
DW D40 ndio nn mkuu?
Kazi yake nn?
 
DW D40 ndio nn mkuu?
Kazi yake nn?
Sorry ni wd40 dawa ya kuondosha kutu au kulainisha vyuma hasa katika gari, maduka ya accesories wanazo hizo. Ukiipata pulizia sehemu nlizokwambia, ukiona bado weka sikio katika mashine katikati ukisikia mlio wa chuma kugonga tambua gari yako ina knock, haraka ipeleke kwa fundi, unaweza kuambiwa ufanye engine overhaul. Kama ni knock itakuwa ina tatizo na oil, either unatumia oil nyepesi sana sana, na kusababisha oil kutofanya kazi yake inavotakiwa au oil ni kidogo sana katka gari yako
 
habari wakuu, hiyo ya mlio wa kugonga kama hodi huwa naisikia karibu mwaka sijawahi ifuatilia kumbe inaweza kuwa ni ishu kubwa hivyo. sorry kwa kudandia uzi
 
Kwanza tazama kama timing billet imesetiwa vizuri pili angalia Plug,tatu tazama petrol filter,nne angalia fuel pump tano, angalia plug cable,kwa hayo machache utajua nini tatizo
 
Habari wakuu.
Nina gari yangu ndogo ninapowasha inatoa mlio mbaya sana kama mashine za kusaga nafaka zile za zamani na inawaka kwa shida mpaka nikanyage mafuta huku nawasha.
Lkn ikiwaka baada ya muda kidogo inatulia.
Msaada wakuu.
Haukufungua starter siku za karibuni
 
habari wakuu, hiyo ya mlio wa kugonga kama hodi huwa naisikia karibu mwaka sijawahi ifuatilia kumbe inaweza kuwa ni ishu kubwa hivyo. sorry kwa kudandia uzi
Ndio mkuu. Inategemea na inavolia, huwa unaanzia mdogo mdogo tu, hata ukenda kwa fundi anaweza kukwambia haina tatizo. Lakini akiwa anausikia sana atakwambia mda umefika.

Knock hutokea kukiwa na detonation kwenye cylinder, au kiurahisi tuseme mripuko kwenye cylinder hutokea kabla ya inavotakiwa. Kawaida ikitokea hii, knock sensor zinapeleka taarifa kwa ECU, ECU hapo inafanya correction ya utiaji mafuta kwenye cylinder kuepusha knock.you need a working O2 sensor kwa hili. Kama sensor ya O2 haifanyi kazi ukimpelekea fundi akutengezee utakua unatia maji kwenye pakacha
 
Taa ya oil inawaka katika dashboard? kibirika chekundu ivi
Habari kaka,

Nadhani ungetoa shule ya bure hata kwa wengine wasioelewa.
Ungewaambia iiwa kibirika kile kinaonyesha hio inaashiria nini.
 
Habari kaka,

Nadhani ungetoa shule ya bure hata kwa wengine wasioelewa.
Ungewaambia iiwa kibirika kile kinaonyesha hio inaashiria nini.
Habari nzuri tu vipina wewe?

Kwenye dashboard kuna vibirika viwili, kimoja kinawaka red chengine ni yellow. Cha yellow kinaashiria kuwa oil level ni ndogo (critical level) au oil temperature is high. Ni vizuri kabla kuwasha gari asubuhi ukatizama oil level yako kabla ya kusepa tu. Taa nyekundu ya kibirika icho inaashiria oil pressure ni low, inasababishwa na oil pump kifeli ama oil pressure sensor kufeli. Ukiendesha gari wakati inawaka utaanza kusikia milio ya vyuma kwenye engine ikisagana, mwisho gari inakuja kusizi (mafundi wanavoita).

Nikiwa pazuri nitakuja kuwaelekeza watu matatizo basic ambayo unaweza kufanya mwenyeo bila kumpelekea fundi na kuwafahamisha kuhusu taa za dashboard
 
Hapo acha kuhangaika peleka gari gereji ikashushwe injini tu huo mlio mara nying hauonaga mbadala wowote zaid ya kubadili mean na con + ring's na cylinder head kit
 
Back
Top Bottom