Mlinzi wa kiwanda auawa akiwa lindoni

Mlinzi wa kiwanda auawa akiwa lindoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
753c8706fe2389442775da129d488ed8

Dar es Salaam. Michael Samwel (23), mlinzi wa kiwanda cha unga cha Lina Miller kilichopo Msongola jijijni Dar es Salaam, ameuawa usiku wa kuamkia jana Alhamisi Mei 2, 2019 lindoni kwake.

Samwel ambaye kawaida analala kwenye kibanda maalumu cha ulinzi, alivamiwa na mtu asiyejulikana na kumtoboa kwa kitu chenye ncha kali.

Sambamba na Samwel, mtu mwingine aliyejeruhiwa kwenye shambulio hilo ni Prosper Haule ambaye ni mfanyakazi wa kiwandani.

Mashuhuda wa tukio hilo wamelieleza Mwananchi Digital leo Ijumaa Mei 3, 2019 kuwa asubuhi ya jana walifika eneo hilo na kukuta Michael kwenye dimbwi la damu.

“Tumeanza kupatwa na hofu kwa kweli tunaamka asubuhi na kumkuta mlinzi amekufa tena ameuawa kinyam, ni jambo la kusikitisha kwa kijana mdogo kama yule,” amesema Bakari Mugitu, mkazi wa Msongola.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ilala, Zuberi Chembela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi.

Amesema uchunguzi wa mwanzo umebaini kuwa mtu aliyefanya mauaji hayo hakuwa na nia ya kuiba chochote zaidi ya kutekeleza akatili huo.

“Inaonekana huyu mhalifu ni mwenyeji maana tumeangalia picha za CCTV anaonekana anavyopanda kwenye ukuta, anavyoingia moja kwa moja mahali alipolala mlinzi na kumchoma kwa kitu cha ncha kali.

“Amemchoma kama mara tano maeneo mbalimbali mwilini, alipomaliza akaondoka bila kuchukua chochote, hii inaweza kuashiria kwamba nia yake ilikuwa ni kufanya ukatili huo tu na alimlenga marehemu,” amesema.

Kamanda Chembela ameeleza kuwa upo uwezekano wa visasi au chuki kuwa sehemu ya chanzo cha mauaji hayo, ila wanaendelea na uchunguzi kupata ukweli.
 
Huyo mlinzi bora amekufa maana asingekufa angeozea jela japo hajashiriki wizi..
Rip soldier pumzika kwa amani
 
Yasemekana ni mlinzi wa pili ndani ya mwezi mmoja katika kiwanda hiko tena wahalifu hao hawachukui chochote.
 
Back
Top Bottom