Mlinzi aliyevunja, kutishia na kubaka afungwa miaka 30

Mlinzi aliyevunja, kutishia na kubaka afungwa miaka 30

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,610
Mahakama ya Wilaya ya Mlele imemuhukumu mlinzi wa Sekondari Ilela, George Sikoki kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa umri wa miaka 16.

Hukumu hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Hakimu Mkazi Mfawidhi Teotimus Swai baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa.

Mwendesha mashtaka, Baraka Hongoli alidai katika ushahidi mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 27 saa 7:30 usiku.

Alidai Sikoki ambaye ni mlinzi wa shule hiyo iliyopo tarafa ya Inyonga wilayani hapa alitenda kosa hilo wakati ambao wazazi wa mtoto huyo wakiwa safirini naye alikuwa akilala peke yake.

Upande wa mashtaka ulidai mshtakiwa alikwenda nyumbani kwa mtoto huyo na kuvunja mlango kisha kumtishia kumuua iwapo angepiga kelele hivyo kumbaka na kutokomea kusikojulikana.

Ilielezwa mahakamani kuwa binti huyo akiwa na maumivu makali, huku akitokwa damu sehemu za siri alijikongoja hadi kwa jirani na kutoa taarifa ndipo alipopelekwa hospitali kwa matibabu.

Hongoli alidai baada ya mshtakiwa kukamatwa alikiri kosa hilo kwa maandishi wakati akihojiwa kituo cha polisi, lakini alipofikishwa mahakamani alikana.

Upande wa mashtaka ulipeleka mahakamani mashahidi sita akiwamo daktari kuthibitisha shtaka hilo ambapo waliithibitishia mahakamani bila kuacha shaka.



Chanzo; mwananchi
 
kama huyo binti atakuwa amepata ujauzito kwa kubakwa... hapo kosa ni la nani!?... huku tena anaambiwa kusoma basi.

tutarajie idadi ya vifo vya kujiua, kutoa mimba, watoto wa mitaani kuongezeka...
 
Miaka 30, kwa utamu wa siku moja? Kweli kichwa cha chini kikishika hatamu, mwanaume hautabaki salama.
Wala sio siku kaka dk1 tu maana cha kubaka unaweza ukaishia mapajani kutokana na unakuwa na mchecheto wa kukamatwa.
 
Mbona wanawake wengi wanasubiri kuombwa tu wanakupa..... Why ubake?
 
Hii biashara ya kukiri police na mahakamani mtu anakana, hapa kuna kitu siyo bure, wakati wa kuhojiwa police watu wawe wanahojiwa wakiwa na wanasheria wao.
 
Hii biashara ya kukiri police na mahakamani mtu anakana, hapa kuna kitu siyo bure, wakati wa kuhojiwa police watu wawe wanahojiwa wakiwa na wanasheria wao.

hapa alipewa kipigo kwanza sio bure
 
Mkumbuke pia wanakwenda jela sio wote wanahatia!!
 
Back
Top Bottom