Mlima warusha majivu kilomita 3 angani Costa Rica

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
160521032835_volcano_ash_covers_costa_rica_640x360_afp_nocredit.jpg

Volkano inaendelea kulipuka katikati mwa Costa Rica, huku ikirusha angani moshi na majivu kwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu.

Mamia ya watu wameenda hospitali wakilalamikia shida ya kupumua na matatizo ya ngozi.

Shule kadhaa nchini humo zimefungwa na safari za ndege kusitishwa au kubadilishiwa njia zinakofuata.

Watu katika mji Mkuu wa San Jose, zaidi ya kilomita 30 kutoka Volcano hiyo ya Turrialba, walisema kuwa majivu yamesambaa kwenye mijengo na magari na kuna harufu kali ya kemikali ya Sulphur.

Shirika la kupambana na maswala ya hatari nchini imewatahadharisha watu kufunika mapua yao na vitambaa vya kujikinga na kuhakikisha wamevaa nguo za kubana ili kukinga mapafu na ngozi zao.

Chanzo:BBC Swahili

Nakumbuka hata volcano la Kilimanjaro ni tuli, siku likilipuka wachaga hawana chao. Tuombe hayo yasitufike!
 
Inakuja kuangamiza watu wanaotaka kuhalalisha ndoa za jinsia moja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom