Mlevi akabwata………….ukifanya tu, kwishnei….!!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Leo mida ya jioni nilitoka na mama Ngina kupata mchesho wa kuku mahali fulani. Mara kaingia mlevi mmoja akasogelea meza yetu na kuniuliza.

“Samahani mzee, naomba uniwe radhi kwa kuuliza”

Mimi nikamwambia uliza tu…………………

Huku akiungalia mkono wangu uliofungwa POP, “eti huo mkono ni ajali au vibaka?”

Nikamjibu ni ajali……………..

Akakunja mkono wa shati lake na kuonesha mkono wake wa kulia ambao ulikuwa na majeraha mengi.

Kisha akasema………….. “mkubwa hii ni ajali, niliuguza huu mkono kwa miezi sita,……… yaani ninavyokuangalia hapo
nakusikitikia…………. Pole sana mkubwa”

Nikamjibu ahsante…………. Akaendelea………… huku akiwa amemgekia mama Ngina………. “samahani shemeji , ukitaka mumeo apone basi kaa naye mbali, maana nyie hamuishi uchokozi, mwenzio mgonjwa, lakini wewe ndio kwanza utamchokonoa mpaka atake, ………..na kama akijaribu kufanya tu……………… hatapona huyu na huo mkono utakatwa”

Watu waliokuwa karibu acha wavunjike mbavu kwa kicheko………………..

Mie na mama ngina tukabaki kutazamana……..

Hakuishia hapo, aliendelea kubwabwaja kilevi, yaani ilikuwa ni burudani.
 
Sasa chagua moja, kupona au kukatwa mkono, hahahaha. Huyu jamaa vere smati!

By the way, umeanza kuona dalili za uchokozi lately?
 
Inasemekana GAME linasababisha vidonda ama majeraha mengine mwilini kuchelewa kupona.Inawezekana alikuwa sahihi.
 
Sasa chagua moja, kupona au kukatwa mkono, hahahaha. Huyu jamaa vere smati!

By the way, umeanza kuona dalili za uchokozi lately?

mbona`uchokozi upo kwa sana tu............. nakufa na tai shingoni
 
afadhali mkuu walau amekufariji na kukupa vunja mbavu. I hope haukukwazika mkuu!
 
kuna swali naogopa kuuliza Mtambuzi. Na hata nikiuliza hapa nadhani naweza kukosa mke humu maana ntaonekana sina maana kabisa, mweeee! Shhhhhhhhhhhhhhhhhhi, taratibu shemeji yenu atasikia anaweza kunipa adhabu ya kuny...........................a naniiiiiiiiii!
 
wanasema walevi na watoto huwa hawaongei uwongo lol

kama ni hivyo iweje mlevi akiongea anapuuzwa na mtoto asikilizwe na kuchuliwa kuwa mkweli kuliko akisema mlevi! na je ushahidi wake unachukuliwa sawa na mtoto mahakamani!
 
Pole kumbe ulipata ajali? by the way fuata ushauri wa huyo mlevi, labda aliona mkao uliokaa na mama ngina ungeweza kukukuruka wakati wowote!
 
Pole kwa ajali pia lisemwalo lipo kama vipi fanyia uchungu kabla hujakukuruka
 
kwa hyo usifaudu mpaka upone mkono? Loh. . .

kwa hili, inabidi tupate ushahidi wa kitaalamu kutoka kwa Dr. Riwa maana sijui kama lina ukweli au ni jambo amblo limepewa nguvu tu na jamii..........
kwangu mimi naona kama moja ya visa asili ambavyo vimetamalaki katika jamii.................
 
Karibu tena Mtambuzi, na pole kwa kuuguza mkono.

Mwambie mama Ngina asikuchokonoe kwa sababu

Ukigusa, kiwishney!
 
Back
Top Bottom