Mkuu wa Wilaya ya Tanga

Mkuu wa Wilaya ya Tanga

victor11

Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
67
Reaction score
7
Mkuu wa wilaya ya Tanga ameamuru afisa elemu wa wilaya akamatwe, kisa wametofautiana misimamo. Je huu ni utawala bora?

Mawazo.

Ni kuhusu majengo yaliyoachwa na mkandarasi aliyejenga barabara ya Horohoro? Nilisikia redioni DC anataka nyumba ziwe za waganga na Afisa elimu anasisitiza kuwa nyumba ziwe za waalimu kwani kiwanja ni cha shule.
 
Habari yenyewe hata haijakamilika. Ungesema wametofautiana nini. Vinginevyo ni vigumu kupima utawala bora kwa tukio moja la mkuu wa wilaya na afisa elimu wake.
 
Mkuu wa wilaya ya Tanga ameamuru afisa elemu wa wilaya akamatwe, kisa wametofautiana misimamo, je huu ni utawala bora !!
Mawazo,
Ni kuhusu majengo yaliyoachwa na mkandarasi aliyejenga barabara ya horohoro? Nilisikia redioni DC anataka nyumba ziwe za waganga na Afisa elimu anasisitiza kuwa nyumba ziwe za waalimu kwani kiwanja ni cha shule.
 
Oooh ni mwendelezo maana jana pia nimeona kwenye News wanafunzi wakilumbana na uongozi wa serikali wakidai nyumba za walimu wao ...... kuna haja ya serikali kutoa tamko nani yupo sahihi
 
Oooh ni mwendelezo maana jana pia nimeona kwenye News wanafunzi wakilumbana na uongozi wa serikali wakidai nyumba za walimu wao ...... kuna haja ya serikali kutoa tamko nani yupo sahihi

Mwenye mamlaka na nyumba hizo nadhani ni waziri wa fedha ambaye ndiye anayeweza kutoa tamko la nani amekabidhiwa nyumba hizo na kwa matumizi yepi. Hospitali ama nyumba za waalimu ni sawa tu kwani vyote ni vya wananchi ila kama zimejengwa kwenye kiwanja cha shule nadhani uongozi wa shule ulikuwa strategic kutoa kiwanja ili wajenzi wajenge kambi na wakiondoka waziache na kuwa mali ya shule. Kama hivyo ndivyo basi mwalimu ana hoja na hakuna haja ya kuamuru akamatwe kibabe.
 
Huyu mama ni mbabe.ni kweli afisa elimu anaitwa sengasu yuko ndani.
 
Si ni vigezo vya USHANGINGI ndio vilizingatiwa!!!! Tanga mnalalamika nini wakati mli waweka madarakani kwa asilimia zaidi ya 90? Ngoja muipate na mtakoma kuringa.
 
waachen wamalizane wenyewee ni mwendelezo tuu wa utawala wa kibabe. hapo mwengne ni mwanasiasa na mwengine ni mfanyakaz wa serikali hyo hyo ya kwetu sikivu!!!!!!
 
Mwenye mamlaka na nyumba hizo nadhani ni waziri wa fedha ambaye ndiye anayeweza kutoa tamko la nani amekabidhiwa nyumba hizo na kwa matumizi yepi. Hospitali ama nyumba za waalimu ni sawa tu kwani vyote ni vya wananchi ila kama zimejengwa kwenye kiwanja cha shule nadhani uongozi wa shule ulikuwa strategic kutoa kiwanja ili wajenzi wajenge kambi na wakiondoka waziache na kuwa mali ya shule. Kama hivyo ndivyo basi mwalimu ana hoja na hakuna haja ya kuamuru akamatwe kibabe.
Hii yote ni sababu ya kuwa na post bila kuwa na majukumu. Mkuu wa wilaya ana kiherehere sio kazi yake kabisa kuamua majengo yaliyoachwa na mkandarasi apewe nani. Mambo ya mali za serikali ni majukumu ya msajili wa Hazina. Inabidi huyu DC aelewe mipaka ya kazi zake, ulinzi shirikishi, masuala ya ulinzi na usalama wa wilaya zaidi ya hiyo hana kazi nyingine.
 
Akiwa mkuu wa wilaya Mpwapwa alikutana na Kaka yangu mmoja kule akiwa ni mtumishi wa Umma ngazi ya Tarafa akamwambia wewe ni mwanamke hutakiwi kuongea mbele yangu alaaah!Maza alifyata mkia japo ni mkuu wa wilaya aka DC...Haya machangu wa JK ukiwaacha watakutekenya mbele ya Mkeo
 
Tatizo mama huyo nimemuona ana akili kama wamama wa magomeni makuti,mwanyamala ukimwambie ukweli atakutukana mpakaaaaaaaaaaaaaa

Na sijui ni kada mzoefu, kwani wakuu wa idara tanga wanamuogopa balah sijui ana kiburi au dharau tu

Mhimu ni kuvundwa tena upya nini maana ya ukuu wa wilaya.
 
Lakini km ni hiyo barabara ya Horohoro, huyo Mkandarasi si alikuwa chini ya Wizara ya Ujenzi (Magufuli)?
Kwa nini Wizara ya afya, Elimu na Serikali na tawala za mikoa wagombanie
Magufuli angeingilia kati kwani fedha za kambi hiyo iliyojenga kwenye kiwanja cha Shule ni za Ujenzi wa barabara.
La sivyo wanafunzi nao waendelee kukomaa
Ni ushauri wangu tu mimi si mkuu wa wilaya au sio Bw Kimbunga
 
Last edited by a moderator:
huyo mkuu wa wilaya ana siku nyingi sasa hajasikika kwenye vyombo vya habari, tangu mwenge ulipopita mwaka jana. mie naona kama vile anataka kujionyesha kuwa naye yupo.
 
huyo mkuu wa wilaya ana siku nyingi sasa hajasikika kwenye vyombo vya habari, tangu mwenge ulipopita mwaka jana. mie naona kama vile anataka kujionyesha kuwa naye yupo.

Nalo neno....

1.Utajuaje kama yupo?
2.Utajuaje kama anafanya kazi?

:help: Tanzania eeeh
 
Back
Top Bottom