Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni aweka wazi mipango yake baada ya ziara yake

josegorofani

Senior Member
Aug 19, 2015
197
69
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Salum Hapi amefanya ziara ya vituo vya Afya vikiwemo Tandale na uwanja wafisi sasa jijini Dar es Salaam na kuweka wazi mipango yake ambayo ameiona akiwa katika ziara hiyo.

Ally Salum Hapi moja ya wakuu wa Wilaya walio na nguvu kubwa haswa ukizingatia aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makondo kupanda cheo na kuwa Mkuu wa Mkoa na aliyafanya mazuri. Hapi ameendeleza mazuri hayo na ameamua kuyatoa yale aliyo yapanga yafanyike baada ya ziara yake.

Mamo liyoyagundua katika ziara yake ni ufinyu wa nafasi kwa kuwa watu wameongezeka katika vituo vya afya, upungufu wa watumishi, uchafu katika vituo na barabara na kwa miundombinu kuchakaa.

Hapi amesema kuwa lazima changamoto hizo zitatuliwe kwa kuungana na watu waliochini yake pamoja na kuhakikisha msongamano wa wagonjwa unapungua katika Hospitali za wilaya.

Aidha amesema kuwa Hospitali ya
Mwananyamala kuandaa mpango wa kujenga majengo mengine makubwa ambapo kuna mkopo waliokopa kwaajili ya kujenga sehemu za kuchomea takataka.
 
Back
Top Bottom