Mkuu wa wilaya kumfukuza kazi mwenyekiti wa mtaa aliyechaguliwa na wananchi. Je ni sawa?

IRINGA MOJA

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
503
229
Nilikuwa naangalia taarifa ya habari Azam Tv na kuona habari ambayo inakichwa cha habari cha "Kibarua chaota nyasi kikaoni" ambako mkuu wa wilaya kamfukuza kazi mwenyekiti wa mtaa katika moja ya mitaa ya Dar katika kikao kilichokuwa na lengo la kutoa elimu ya mambo ya kodi kilichoratibiwa na TRA huku mkuu wa wilaya ya Ilala akiwa mgeni rasmi. Sababu ya kufukuzwa mwenyekiti huyo ni mkuu huyo wa wilaya kuhisi amezihakiwa na kufanyiwa utani katika majukumu yake ya kikazi na mwenyekiti huyo.

Kwa hali hii hivi inakuwaje mtu aliyechaguliwa na mamia U maelfu ya watu akafukuzwa kiholela hivo na mtu aliyeteuliwa kwa fadhila za mtu mmoja?
 
Hakufukuzwa kazi,bali alimfukuza kikaoni na kuamuru atolewe,lakini huyo mwenyekiti aliomba radhi akaambiwa aandike barua ya maelezo.
Ndio maana shule umefeli wewe
 
Sawa mkuu, hongera wewe uliyefaulu na kufanikiwa kimaisha
 
Mwenye kuitisha kikao anamalaka ya kumtoa nje/kumwondoa Mjumbe asiyemtaka.
 
Viongozi wa kuteuliwa wa zama hizi wanashangaza sana; wanawaona viongozi wa kuchaguliwa kama watumishi wa umma. Hawajui kuwa hawa ni viongozi wa jamii wanaopaswa kuheshimiwa muda wote. Sijui hawa watu wameokotwa wapi.
 
Back
Top Bottom