Mkuu wa wilaya Dr. Norman Sigalla awatusi walimu Mbeya.

Vunjavunja

Member
May 18, 2012
92
11
Ualimu ni fani ya watu waliofeli, hivyo hawana haki ya kudai nyongeza ya mishahara, hii ni kauli ya mkuu wa wilaya Mbeya Dr. Norman Sigalla huu ni uzalilishaji wa fani ya ualimu, na kudhalilisha fani zote hata yeye mwenyewe maana hata kuteuliwa kwake na J.K wote walifundishwa na walimu nina mashaka na Dr wote huenda ni kama wa J.k au wa kuiba vyeti mtu msomi hawezi kusema hivyo.
 
Una point ila tulia uandike vizuri asije akakutukana na wewe
 

Rekebisha heading basi!
 

walimu wa tanzania walishajitukana wenyewe, kwa kuibeba ccm. huyo jamaa anarudia tu.
 
Kama kweli kasema maneno hayo, hastahili kutetewa. Ulimbukeni. Ujinga wa kifikra ni mbaya sana maana hata ukipata PhD bado haiondoi matatizo yako. Sio PhD zote ni za kweli. Feki ziko nyingi sana siku hizi na hizo ndo zinasumbua sana. Wanaostahili PhD huwezi kuamini hawajichomekei sana na upuzi. Hata ukiambiwa unaweza kukataa. Lakini wanunuzi wa PhD wanapiga domo chafu lenye harufu mbaya utashangaa! Poleni watu wa Mbeya, huyo ndiye kiongozi wenu mnayemtazamia kuwafanya mpige hatua kwenda mbele. Imekula kwenu. JK kawachomekea sababu anajua hana kitu tena kutoka Mbeya, ndiyo maana anawalimboka, anawadaudi, anawakyembe, anawandosya,.....sijui nitaje yote? Masikini banyambala. Poleni. Amkeni sasa mjue namna gani mnatakiwa kuishi. CCM sio mama yenu.
 
kama ww ni mwalimu basi kweli hii fani ya watu waliofeli manake hii heading tu umeshindwa kuiandika kwa kiswahil fasaha sasa kwa nn tusisema kuwa ulifeli?
 

Inaandikwa na kutamkwa WILAYA na sio WIRAYA!
 
Vipi au wewe ndo mwenyewe hujui maana ya nukuu kama huna la kuchangia kaa kimya sisi ndo walimu ambayo elimu yetu ni ya uhakika si ya kupewa mezani tumeangaika na elimu ya kitanzania, na tunadhalilishwa na watu wa vyeo vya kuteuliwa.
 
OK, tuangalie hoja yake, hizo typographic errors haziondoi umuhimu wa story. Mezea hiyo na endelea na kuchangia the core issue. Labda Vunjavunja alikuwa na hasira sana alipokuwa anaandika story, hata wewe bila shaka imewahi kukutokea kuandika herufi ambayo hukuimaanisha. Kubonyeza pembeni ukakuta umetukana mtu fulani.
 
Inaonesha viongozi hawa ndo vyanzo vya kuleta migogoro ktk jamii zetu anatakiwa kuomba msamaha kwa walimu wote wa tanzania si wa wilaya ya mbeya tu.
 
kama ww ni mwalimu basi kweli hii fani ya watu waliofeli manake hii heading tu umeshindwa kuiandika kwa kiswahil fasaha sasa kwa nn tusisema kuwa ulifeli?

Nakubaliana nawe kwani acha heading hata mpangilio wa content, wilaya kaandika wiraya. Kama ni mwalimu kazi ipo TZ. sijui tunazalisha kizazi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…